Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Viongozi wa Umma mkoani humo,
wakati akifungua mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni
03, 2019 Mjini Bariadi.
Baadhi ya
Viongozi wa Umma mkoani Simiyu wakifuatilia
mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili yao na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni
03, 2019 Mjini Bariadi.
Kaimu Katibu
Msaidizi Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora,
Bw. Gerald Mwaitebele, akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, wakati wa
mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi hiyo, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini
Bariadi.
Hakimu
mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio akichangia hoja
wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu,
ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo akichangia hoja wakati wa
mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo
yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
.....................
Na Stella Kalinga,
Simiyu
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu amesema ni vema Sekreatarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma
iendelee kuwakumbusha viongozi na watumishi wa umma nchini kutimiza wajibu wao
ili kuweza kufikia malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli na Serikali.
Mtaka
ameyasema hayo Juni 03, 2019 Mjini Bariadi, wakati akifungua mafunzo kwa
Viongozi wa Umma mkoani Simiyu, ambayo yameandaliwa na Ofisi ya Rais
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora.
Amesema
ikiwa kila mmoja katika Utumishi wa Umma atatimiza wajibu wake jamii na nchi
kwa ujumla wake itaweza kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali katika nyanja
mbalimbali kwa wakati.
“Ni
vizuri Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ikiendelea kuwakumbusha watu
wote wanaofanya kazi zinazoihusu jamii kutimiza wajibu wao, kila mmoja
akitimiza wajibu wake yapo mambo mengi sana sisi kama jamii, nchi, mkoa na kwa
namna ambavyo uongozi na mgawanyiko wa .nchi yetu ulivyo tutafikia malengo yetu
kwa wakati” alisema Mtaka.
Aidha,
ametoa wito kwa viongozi wa Umma ambao ni watoa maamuzi katika maeneo yao ya
kazi kuwa makini katika kutoa maamuzi na wahakikishe wanafanya maamuzi kwa
wakati.
Kwa
upande wake Kaimu Katibu Msaidizi Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Gerald Mwaitebele amesema viongozi wa Umma
wanapaswa kutoa maamuzi kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo
iliyowekwa ili kutoiletea hasara Serikali.
Ameongeza
kuwa Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Umma itaendelea kutoa elimu kwa
viongozi wa umma juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi ya uadilifu katika
uongozi na endapo ikitokea kiongozi yeyote atakengengeuka na kutofuata maadili
sheria itachukua mkondo wake.
Kwa
upande wake Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio
ameshukuru Sekretarieti ya Maadili kwa kutoa mafunzo ya maadili kwa viongozi wa Umma na akatoa wito kwa
viongozi hao kuwa waadilifu, kutekeleza majukumu yao na kutojilimbikizia mali
kinyume na taratibu na maadili ya viongozi wa Umma.
Naye
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Bahame Kaliwa
ametoa wito kwa Sekretarieti ya Maadili kwa viongozi wa Umma kutoa elimu ya
maadili kila viongozi wapya wanapoteuliwa au kuchaguliwa, hususani madiwani
wanapochaguliwa na kuunda Mabaraza mapya ya madiwani ili wajue misingiya
uadilifu inayopaswa kuwaongoza katika kazi zao
No comments:
Post a Comment