Wednesday, June 12, 2019

RAIS WA DRC KONGO KUTUA NCHINI KESHO KWA ZIARA YA KIKAZI NA KUPOKELEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. JOHN MAGUFULI

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi kesho Juni 13 anatarajia kufanya ziara ya kikazi kwa siku mbili nchini Tanzania na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli.
Akitoa taarifa ya ugeni huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema Rais Felix Tshisekedi atawasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Majira ya Mchana na baada ya kuwasili ataelekea Ikuku Dar es salaam ambapo atafanya mazungumzo na Rais Dkt. John Magufuli kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo jinsi ya kuimarisha uchumi na maendeleo.
RC Makonda amesema ugeni wa viongozi mbalimbali nchini ni matokeo ya uongozi imara na thabiti wa Rais Dkt. John Magufuli katika usimamizi wa Amani, usalama, maendeleo na uwepo wa diplomasia imara

No comments:

Post a Comment