Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim
Wangabo (kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa afisa wa TBA Haruna
Kalunga (kulia) wakati alipotembelea ujenzi wa ofisi ya Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya kalambo.
***********************************************
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mh.
Julieth Binyura amemkaribisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kalambo katika ofisi yake mpya anayotarajia kuhamia mwishoni mwa mwezi
wa sita mwaka 2019 huku ikiwa zimebaki asilimia 10 kumalizika kwa jengo
hilo tofauti na ofisi ya mpya ya Mkurugenzi ambayo bado ipo katika hatua
za awali za ujenzi.
Mh. Binyura aliwashukuru
wakandarasi Suma JKT pamoja na mshauri wake wakala wa majengo Nchini
(TBA) kwa kuweza kuifikisha ofisi hiyo katika hatua za mwisho kuongeza
kuwa pamoja na yeye kuhamia pia anaweza kushirikiana na mkurugenzi kukaa
pamoja ikiwemo kumuazima mabanda yanayozunguka ofisi hiyo ili aweze
kuyatumia wakati wakisubiri kukamilisha ofisi yao.
“Ni kweli jengo hili ni kubwa sana
na ofisi hii itatosha kwa ofisi yangu pia na Mkurugenzi ataingia na pia
kuna mabanda mengi tu yapo hatutayabomoa mapema ili waweze kuingia
lakini vile vifaa ambavyo ni vya kutumia mifumo wataingia kwenye jengo
langu, kwahiyo nawakaribisha sana na wajenzi wajitahidi ili tarehe 30
niweze kuingia kwenye jengo hili,” alisema.
Kauli hiyo imekuja baada ya mkuu
wa mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo kumtaka Mkurugenzi wa halmashauri
hiyo kuhama katika madarasa ya shule ya Sekondari ya wasichana Matai
ambayo wanayatumia kama ofisi zao.
Mh. Wangabo alisema,” Mh. DC
nimesema hawa halmashauri ofisi zao zitahamia kwako kwa muda utakapokuwa
umehamia pale na pale uwape muda wa kukaa ili uwasukume watoke pale,
kama hawatasimamia huu ujenzi hapa wake kule kwenye vibanda vya kuku
kule,wakae kweny vibanda vya mabati ili waone uchungu wa kusimamia hapa
mahali.
Mh. Wangabo aliyasema hayo
alipotembelea ujenzi wa ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Ofiri ya
Mkurungenzi wa halmashauri pamoja na ujenzi wa bwalo na mabweni katika
Shule ya Sekondari ya Wasichana Matai.
Katika hatua nyingine Mh. Wangabo
amemuagiza Mkurugenzi wa halmashauri ya Kalambo kuhakikisha hadi kufikia
mwezi Julai mwaka 2019 shule hiyo iwe imesajiliwa na kuanza kupokea
wanafunzi kutoka katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Tangu kuanzishwa kwa halmashauri
hiyo mwaka 2012 Mkurugenzi amekuwa akitumia madarasa ya shule ya
sekondari ya wasichana ya Matai kama ofisi za halmashauri.
No comments:
Post a Comment