Friday, June 21, 2019

NAIBU MEYA JOSEPH LYATA ATATUA TATIZO LA BARABARA YA DODOMA ROAD

NAIBU Meya Manispaa ya Iringa Joseph
Lyata kwa kushirikiana na Chama cha Mapinduzi CCM Manispaa wameendelea
kutekeleza ahadi ya kukarabati za Mitaa iliyopo kata ya Mtwivila kama ambavyo unawaona hapo kwenye picha

NAIBU Meya Manispaa ya Iringa Joseph
Lyata akiwa anaangalia ukarabati barabara za Mitaa iliyopo kata ya Mtwivila

Baadhi ya watoto na wananchi wakiangalia ukarabati wa barabara ukiendelea katika mitaa ya kata ya Mtwivira

 

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

NAIBU Meya Manispaa ya Iringa Joseph
Lyata kwa kushirikiana na Chama cha Mapinduzi CCM Manispaa wameendelea
kutekeleza ahadi ya kukarabati za Mitaa iliyopo kata ya Mtwivila.

Akizungumza na wananachi wa Mtaa wa
Dodoma Road C wakati wa kukarabati barabara hizo, Lyata amesema kuwa wameamua
kukarabati barabara hiyo kutokana na ubovu uliokuwepo awali.

Lyata amesema kuwa anashangaa kuona
Diwani wa kata ya Mtwivila kushindwa kukarabati barabara za mitaa hiyo huku
akiwataka wananchi wa Kata hiyo kutoa taarifa katika ofisi yake na kuendelea
kutatua changamoto zinazowakabili.

Awali Lyata amebainisha kuwa Chama
cha mapinduzi kimekuwa kikiwafikia wananchi wa chini na kujua changamoto zao na
kisha kuzitatua.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa
DODOMA ROAD C Mzee Said Mwachang’a amemshukuru naibu meya manispaa ya iringa Joseph
Lyata kwa kuwarekebishia barabara hiyo kwani itafungua fursa ya wafanyabiashara
kufika katika mitaa yao.

“Nikushukuru Naibu meya kwa kuja kutekeleza
ilani ya chama cha mapinduzi kwani umeonesha wewe ni kiongozi wa watu na
tunakupongeza kwa hili” alisema Mwachang’a

Nao baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Dodoma
Road C wamebainisha kuwa baada ya ukarabati wa barabara hiyo utapelekea waweze
kufanya shughuli zao bila tatizo.

Lakini diwani wa
kata ya Mwangata Nguvu Chengula alisema kuwa chama cha mapinduzi na naibu meya
wa manispaa ya Iringa walikuwa hawalali kwa ajili ya kutatua tatizo la barabara
ya Dodoma Road  kwa kuwa wananchi hao wanahitaji kufanya kazi za
kimaendeleo

“Wananchi wa kata
ya Dodoma Road wanahitaji kufanya maendeleo kwa kuwa wamekuwa wachapa kazi
wakubwa lakini mbunge wao amekuwa hawasaidie kwa lolote hivyo ndio chama na
Naibu Meya walipobebe jukumu la kutatua changamoto hiyo” alisema Chegula

Chegula alisema
kuwa kipaumbele kilikuwa kutatua changamoto ya barabara ndipo wanatafuta njia
nyingine ya kutatua changamoto nyingine zilizopo katika mtaa wa Dodoma Road ili
wananchi wafanye kazi kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anavyotaka.

No comments:

Post a Comment