MIKOA YA DAR NA TANGA YATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WANACHI KUANGAMIZA MAZALIA YA MBU
Ziara
yaWaziri wa afya Ummy Mwalimu,Naibu Waziri wake pamoja na viongozi
mbalimbali mkoa wa DSM wakikagua eneo la jangwani katika mkakati wa
kupulizia dawa za kuua mazalia ya mbu ili kukabiliana na homa ya dengue
kwa mkoa huo
…………………
Na.WAMJW,Dar es Salaam
Mikoa
ya Dar es Salaam na Tanga imetakiwa kushirikiana na wananchi kuangamiza
mazalia yote ya mbu kwa kunyunyizia dawa za kuua mbu wapevu kwa
kutumia mashine kubwa.
Hayo
yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu wakati alipotembelea eneo la jangwani jijini hapa.
Waziri
Ummy amefanya maamuzi haya baada ya mikoa hiyo kuathiriwa na ugonjwa wa
homa ya Dengue”nimeelezwa mkoa wa Dar es Salaam unahitaji kununua lita
1000 za dawa aina ya Acteric 500 na Icteric 300 kwa ajili ya kunyunyizia
mbu wapevu katika mitaa,ninawataka wakurugenzi wa Manispaa kuhakikisha
dawahizi zinanunuliwa mara moja na.kufanya upuliziaji katika maeneo
yenye mbu”Alisisitiza Wazirj Ummy.
Aidha,
amewataka wamiliki na waendeshaji wa
migahawa,bar,mahotel,saluni,gareji,mashule,maofisini na sehemu zote
zinazozunguka maeneo yao wanakagua mazalia ya mbu,kufukia madimbwi ya
maji na kufanya usafi kwa ajili ya kuangamiza mazalia ya mbu.
Hata
hivyo alivitaka vituo vya kutoa huduma za afya vikiwemo vya watu
binafsi kuzingatia taratibu na miongozo iliyopo ya kutoa taarifa kwa
uongozi wa afya wa halmashauri kila siku wanapopima na.kugundua kuwa ntu
ana ugonjwa wa dengue bila kuacha.
Wakati
huohuo Naibu Waziri Dkt.Faustine Ndugulile amewataka watoa huduma za
afya ambao sio waaminifu kutotoa majibu yasiyo sahii ya dengue na kutoa
dawa zisizostahili kwa ugonjwa huu
“Tutaanza
kuchukua hatuakali kwa watu wanaojirekodi na kusambaza klipu zinazosema
watu wanywe maji ya mipapai au kupaka mafuta ya nazi ,tunasema ugonjwa
huu hauna tiba hivyo mtu yeyote anayeona ana dalili hizo ni kufika kituo
cha afya “Alisema Dkt.Ndugulile
Naye
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Abubakari Kunenge amesema kama
mkoa watatekelza maagizo yote na kuteketeza ugonjwa huo hivyo
kuhakikisha wanaanza kupuliza dawa kwenye maeneo ya mazalia na kutoa
wito kwa wananchi kushirikiana kufanya usafi wa mazingira na kuondoa
mazalia ya mbu kwa ustawi wa afya
No comments:
Post a Comment