MHE.MGALU AWASHA UMEME VIJIJI VYA BICHA,KOLO NA KWAYONDU KONDOA MKOANI DODOMA
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu
akizungumza na wananchi wa kata ya Kilimani wilayani Kondoa kabla ya
kuwasha umeme katika Shule ya Sekondari Bicha.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu
(katikati) akikata utepe kuashiria umeme kufika kwenye Shule ya
Sekondari ya Bicha wilayani Kondoa.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu
akiwasha umeme katika Shule ya Sekondari ya Bicha iliyopo kata ya
Kilimani wilayani Kondoa.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu
akizungumza na wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne katika Shule
ya Sekondari ya Bicha mara baada ya kuwasha umeme.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu
akicheza na wananchi wa kijiji cha Kolo mara baada ya kuwasili kuwasha
umeme katika Zahanati ya Kolo wilayani Kondoa.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu
akizungumza na wananchi katika Zahanati ya Kolo wilayani Kondoa kabla ya
kuwasha umeme katika zahanati hiyo.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu
(katikati) akikata utepe kuashiria umeme kufika kwenye Zahanati ya Kolo
wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwasha umeme katika Zahanati ya Kolo iliyopo wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu
akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Kwayondu wilayani Kondoa huku
akiwa ameshika kifaa cha umeme Tayari (UMETA) akiwapa elimu ya kutumia
umeme huo kabla ya kuwasha umeme katika Kijiji hicho.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizindua umeme kuashiria kufika katika kijiji cha Kwayondu wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu
akiwasha umeme katika shule ya Sekondari ya Kwayondu iliyopo kijiji cha
Kwayondu wilayani Kondoa Mkoani Dodoma.
………………….
Na.Alex Mathias,Kondoa
Naibu Waziri wa Nishati Mhe.Subira Mgalu
amefanya ziara ya kuwasha umeme katika wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma
ambapo amewasha katika Shule ya Sekondari Bicha,Zahanati ya Kolo pamoja
na kijiji cha Kwayondu ikiwa ni juhudi za Serikali za kuhakikisha kila
mwananchi aweze kuunganishiwa umeme.
Mhe.Mgalu amesema kuwa, kuwashwa kwa
umeme katika vijiji hivi ni muendelezo wa utekelezaji wa adhma ya
Serikali ya Awamu ya Tano kufikisha umeme katika Vijiji vyote nchini.
Aidha Mgalu akizungumza
na wananchi huku akitoa elimu kuhusu gharama za kuwaunganishia umeme
amesema Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli inawajibu ya
kuwajali na kuwathamini wananchi wa kipato cha chini.
Amesema kuwa Serikali imeamua kushusha gharama za kuwaunganishia umeme wananchi wake hadi shilingi 27,000/= tu.
“Hapo mwanzo gharama za
kuunganishiwa umeme zilikuwa ni shilingi 177,000, lakini Serikali kwa
vile inawajali wananchi wake imelipa shilingi 150,000/= kwa kila
anayeweka umeme, na kazi ya mwananchi ni kulipia kiasi kidogo tu cha
shilingi 27,000/=, tofauti na hapo awali.” amesema Mhe.Mgalu
Hata hivyo Mhe.Mgalu, pia amesisitiza
wananchi kutumia vifaa vya Umeme Tayari (UMETA) ambavyo vitawawezesha
kuondokana na gharama za wiring na kuwezesha kuunga wateja wengi .
“Gharama hizo za wiring
zimeonekana kuwa ndio changamoto kwa wananchi na serikali imepokea
changamoto hizo na kuwa itazifanyia kazi.” amesisitiza
Naibu Waziri huyo ameutaka uongozi wa
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Dodoma na Kondoa kuhakikisha
wanakamilisha usambazaji wa umeme kwa wanakijiji ili waweze kunufaika
na huduma hiyo.
No comments:
Post a Comment