Mwenyekiti
wa kamati ya mashindano ya Ritta Kabati Gerald Malekela akitoa maelezo
kwa viongozi wa timu shiriki kwenye mashindano ya Ritta Kabati Challenge
Cup msimu wa tatu 2019
Baadhi ya viongozi wa timu shiriki kwenye mashindano ya Ritta Kabati Challenge Cup msimu wa tatu 2019 wakiwa makini kusikiliza maelezo kutoka kwa mwenyekiti wa mashindano.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Jumla ya timu thelethini na
sita (36) za mkoani Iringa kushiriki mashindano ya Ritta Kabati Challenge awamu
ya tatu 2019 katika viwanja mbalimbali ya mpira wa miguu mkoani Iringa ambapo
mashindano hayo yanatarajiwa kuzinduliwa siku ya jumamosi tarehe 15 / 06 /
2019.
Akizungumza na waandishi wa
habari mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Ritta Kabati Gerald Malekela
amesema kuwa timu zilizoshiriki mashindano hayo zinatoka katika wilaya ya Mufindi,Kilolo
na Iringa hivyo inajumuisha wilaya zote za mkoa wa Iringa.
“Kwa mara ya kwanza tumepata
timu nyingi kutoka katika halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini kwa
kujitokeza timu kumi na moja hiyo inaonyesha jinsi gani kila kukicha mashindano
haya yanazidi kuwa na mvuto na ushindani unaongezeka” alisema Malekela
Malekela alisema msimu huu
mashindano yatakuwa bora kuliko misimu iliyopita kwa kuwa kamati imejipanga
kuhakikisha wanatengeneza kitu kilicho bora na kuongeza thamani ya mashindano
na kuweka alama ya kuigwa kwa wapenda michezo hasa mchezo huu wa mpira wa miguu.
“Tumejipanga kwelikweli
kuhakikisha kuwa mashinda haya yanakuwa ya kiwango cha hali ya juu kiasi kwamba
kila mtu atakuwa anavutiwa na mfumo wetu ambao tumekuwa tunautumia kuendesha
mashindano haya” alisema Malekela
Malekela alisema kuwa lengo la
mashindano hayo ni kukuza na kuibua vipaji vya wachezaji kutoka ngazi ya chini
hadi kwenda kucheza ligi ambazo ni rasmi kama vile ligi daraja la kwanza la
pili pamoja na ligi kuu katika nchi mbalimbali.
“Mwaka jana tulifaulu kwa
kuhakikisha kuwa vijana wengi waliocheza mashinda haya walisajiliwa kwenye
vilabu mbalimbli kuanzia ligi kuu hadi madalaja ya chini hivyo hayo nayo
yalikuwa mafanikio makubwa kwetu” alisema Malekela
Aidha Malekela alisema kuwa
mashindano hayo yamekuwa yakikumbwa na changamoto ya ubovu na uhaba wa viwanja
vya mpira wa miguu,hivyo tunaiomba serikali kuhakikisha wanatusaidia kuboresha
viwanja hivyo
No comments:
Post a Comment