HASSAN KESSY ARUHUSIWA KUICHEZEA TAIFA STARS DHIDI YA SIMBA WA TERENGA JUMAPILI
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF),
limemruhusu beki wa timu ya soka ya taifa Taifa Stars,Hassan
Kessy,kucheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Senegal,utakaofanyika Juni
23,katika Uwanja wa 30 June Cairo,nchini Misri.
Maamuzi hayo ya CAF ya kumruhusu Kessy
kucheza mchezo dhidi ya Senegal ni baada ya kujiridhisha,kuwa kadi mbili
za njano, ambazo zilikuwa awali zinasemekana zingemfanya asicheze
mchezo huo zilishaisha katika mchezo namba 101 ambao ulikuwa ni dhidi
Cape Verde nyumbani.
Kutokana na taarifa hiyo ,Kocha Emmanuel
Amuneke,anaweza kumtumia Kessy katika mchezo huo wa kwanza wa kombe la
Mataifa Afrika (AFCON) bila tatizo lolote kama atakuwa yupo kwenye
progarmu yake.
Ikumbukwe kuwa.kesi alipata kadi mbili za
njano katika michezo miwili ya ugenini dhidi ya Uganda Cranes na Cape
Verde,ambazo zilimalizika na kumfanya adhabu yake ya kutocheza iweze
kuisha baada ya kusimama namba 101.
No comments:
Post a Comment