Daktari katika mpaka wa Tanzania
na Kenya kwenye eneo la Namanga, Anna Anthony, akiwapima wasafiri
wanaopita katika mpaka huo, wakati wa zoezi la Kupima Utayari wa nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na magonjwa ya
mlipuko mipakani, leo tarehe 13 Juni, 2019.
Mtaalamu wa Afya akimhudumia
mmoja wa wasafiri waliokuwa wakipita katika mpaka wa Tanzania na Kenya,
kwenye eneo la Namanga aliyeigiza kuugua, wakati wa zoezi la Kupima
Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kukabiliana na
magonjwa ya mlipuko mipakani, leo tarehe 13 Juni, 2019.
*****************************
Kufuatia zoezi linaloendelea
mpakani mwa Tanzania na Kenya kwenye eneo la Namanga, ambalo linajikita
katika Kupima Utayari wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Kukabiliana na magonjwa ya mlipuko mipakani, leo tarehe 13 Juni, 2019,
Wataalamu wa sekta za Afya wa Tanzania na Kenya, katika makundi tofauti
wameweza kutekeleza kwa vitendo kwa kutumia Dhana ya Afya moja katika
Kupima kwa vitendo hatua za kujiandaa na kukabili Ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa.
Wataalam hao wameweza
kutathmini uwezo wa uchunguzi na usimamizi wa wagonjwa wa Homa ya Bonde
la Ufa mpakani, pamoja na kufanyia majaribio ya utekelezaji wa Mipango
ya Dharura ya Taifa na Kanda, Miongozo ya Utendaji katika kukabili na
kupunguza madhara ya ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa kwa Wanyama na
Binadamu.
Zoezi hilo, linazingatia Dhana
ya Afya moja ambayo hujumuisha sekta ya afya ya binadamu, wanyamapori,
mifugo na mazingira katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa
yanayoathiri binadamu.
No comments:
Post a Comment