BAADA YA KUCHEMSHA KWENYE FAINALI LIGI YA MABINGWA ,CAF YAITISHA KIKAO CHA DHARULA
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjz4XqwBx0XWe4y6mu0M0BJj5CRFxS90wVQe0Fl0UxOKbNtKfAsQj4eALq_39eal4xDklTvAAQKUovlyO2WrgdUgG7DI-FrLIXEd_DH9drrACWpzjiLYmqU0k-nS4ygtBbe9vF3TdVaJiQl/s1600/espearance.jpg)
Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika
CAF, Ahmad Ahmad ameitisha kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya
shirikisho hilo kufuatia sintofahamu katika mchezo wa pili wa fainali ya
Klabu Bingwa Afrika.
Mei 31 nchini Tunisia kati ya wenyeji
Esperance de Tunis na Wydad Casablanca ya Morocco mchezo uliisha kwa
sintofahamu kufuatia klabu ya Wydad kugomea kuendelea na mchezo baada ya
bao lao la kusawazisha kukataliwa katika dakika ya 62 ya mchezo.
Taarifa ya CAF imesema kuwa kikao hicho
kitafanyika Juni 4, ambapo ajenda kuu itakuwa ni juu ya sheria
zanazopaswa katika kutatua sintofahamu ya mchezo huo.
Kwenye mchezo huo, Wydad walisawazisha
bao, ambalo lingeufanya mchezo kuwa sare ya 1-1 lakini mwamuzi alikataa
bao hilo na halikurudiwa katika teknolojia ya usaidizi wa video VAR kwa
kile mwamuzi alichokidai kuwa mashine kuharibika.
Baada ya Wydad kugoma kuendelea na
mchezo, mwamuzi alimaliza mchezo na kuipa ushindi wa bao 1-0 klabu ya
Esperance pamoja na ubingwa wa michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment