Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akiongoza kikao kazi cha majumuisho ya ujumbe kutoka Benki ya Dunia kuhusu ufuatiliji wa utekelezaji wa Mradi wa kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga (Expanding Rice Production project), Kilichofanyika Jijini Dar es salaam tarehe 22 Mei 2019.
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akiongoza kikao kazi cha majumuisho ya ujumbe kutoka Benki ya Dunia kuhusu ufuatiliji wa utekelezaji wa Mradi wa kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga (Expanding Rice Production project), Kilichofanyika Jijini Dar es salaam tarehe 22 Mei 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam
Katibu Mkuu wa Wizara
ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe ameengoza kikao kazi cha majumuisho ya
ujumbe kutoka Benki ya Dunia kuhusu ufuatiliji wa utekelezaji wa Mradi wa
kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga (Expanding Rice Production project),
mradi ambao unatekelezwa Tanzania bara na Zanzibar.
Kikao hicho cha
majumuisho kimefanyika leo leo Tarehe 22 Mei 2019 katika ukumbi wa ofisi ndogo
za Wizara ya Kilimo maarufu kama Kilimo 1 Jijini Dar es salaam.
Ujumbe huo kutoka
Benki ya Dunia ukiongozwa na Bi Sarah Simons umeeleza kuridhishwa na kasi ya
utendaji kazi katika utekelezaji wa kazi za mradi huo kulingana na malengo
yaliyowekwa kwa kipindi cha miezi 6 iliyopita.
Ujumbe huo ulianza kazi
ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Mradi huo
wa ERPP tarehe 19-21 Mei 2019 ambapo walitembelea Tanzania bara na
Zanzibar na walikutana katika wizara ya Kilimo (Bara) na Wizara ya kilimo, Maliasili, Mifugo na
Uvuvi (Zanzibar) na wameshukuru ushirikiano walioupata kwa watendaji
wanaosimamia mradi huo.
Aidha ujumbe huo pamoja na kusisitiza kasi ya utekelezaji na ukamilishaji wa kazi za Mradi
huo pia waliridhishwa na namna ambavyo mradi umekuwa ukiripoti kuongezeka kwa
uzalishaji wa mpunga kwa hatua za awali baada ya wakulima kutumia mbegu bora
katika mfumo wa kilimo shadidi (SRI).
Pia maendeleo mazuri
katika maandalizi ya ujenzi wa miundombinu ya Umwagiliaji na Maghala kwa
kipindi cha miezi sita iliyopita na wamekuwa na matumaini kuwa Ujenzi wa miradi
hiyo na kazi zingine zitakamilika kabla ya tarehe ya mwisho ya mradi huo.
Mhandisi Mtigumwe
(Katibu Mkuu Kilimo Tanzania bara) ameushukuru ujumbe huo na kuwaeleza kuwa
wataendelea kwa kasi kutekeleza shughuli zilizobaki za mradi huo ili tija kwa
wakulima na nchi ionekane.
Kwa upande wake Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Maliasili, Mifugo na Uvuvi Bi Mansura Kassim aliushukuru
Ujumbe huo kwa ufuatiliaji wao na kueleza kuwa Kwa upande wao wataendelea
kukamilisha kazi zilizobakia katika mradi na kusimamia mradi huo ipasavyo.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment