Madiwani
wa halmashauri ya Wilaya ya Ileje wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Songwe
Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela (hayupo pichani) katika kikao ambapo
walitoa malalamiko ya kutoridhishwa na utendaji wa Mkurugenzi wa
halmashauri ya Ileje.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
(Mst) Nicodemus Mwangela (katikati) akiwasikiliza madiwani wa
halmashauri ya Wilaya ya Ileje (hawapo pichani) katika kikao ambapo
walitoa malalamiko ya kutoridhishwa na utendaji wa Mkurugenzi wa
halmashauri hiyo, Kulia kwake ni Katibuwa CCM Mkoa wa Songwe Mercy
Mollel na Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje
Ubatizo Songa.
*****************************
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen.
(Mst) Nicodemus Mwangela ameunda timu ya kuchunguza tuhuma 13 zilizo
elekezwa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje na kuelekeza kuwa timu
hiyo ifanye uchunguzi huo kwa haraka.
Brig. Jen. (Mst) Mwangela amefikia
uamuzi huo mara baada ya majadiliano ya kikao cha pamoja na madiwani wa
Halmashauri ya Wilaya ya Ileje waliomuandikia barua wakiwasilisha
tuhuma za kutoridhishwa na utendaji wa Mkurugenzi huyo.
“Nimefanya ziara Wilaya ya Ileje
baada ya kupata barua kutoka kwa Madiwani wakimtuhumu Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Ileje, kabla ya kufanya maamuzi tumejadiliana na
nimefikia uamuzi wa kuunda tume ambayo itachunguza tuhuma zote 13
walizowasilisha”, ameeleza Brig. Jen. (Mst) Mwangela.
Amesema kazi kubwa ya tume hiyo ni
kuhakikisha wanapata ukweli na uhalisia juu ya tuhuma hizo huku
akielezea kuwa moja ya tuhuma ni udhaifu katika kukusanya mapato.
“Kuna tuhuma ambazo tunaona zina
ukweli mfano Ileje haijafanya vema katika suala la ukusanyaji wa mapato,
sasa tumebakiza mwezi mmoja mwaka wa fedha uishe lakini wamefikia
asilimia 58 tu ya makusanyo ambapo ni asilimia ndogo ikiwa lengo ni
angalau zaidi ya asilimia 80 kwahiyo hapo kuna dalili za uvujishaji wa
mapato”, Amefafanua Brig. Jen.(Mst) Mwangela
Brig. Jen. (Mst) Mwangela
ameongeza kuwa licha ya kwamba uchunguzi unaendelea ametoa maelekezo na
mikakati ambayo itasaidia kuhakikisha kazi ya ukusanyaji wa mapato
inaendelea vizuri.
“Lengo ni kukusanya vizuri kwahiyo
katika kikao tumeweka mikakati itakayosaidia kukusanya mapato na tuna
amini waendaji wote wa halmashauri ya Wilaya ya Ileje watafanya kazi kwa
umakini mkubwa huku kamati ya fedha na mipango ya madiwani itasimamia
hilo vema”, amesema Brig. Jen. (Mst) Mwangela.
Baadhi ya tuhuma ambazo Madiwani
wamezielekeza kwa Mkurugenzi wa halmashauri ni pamoja na matumizi mabaya
ya ofisi na tuhuma katika masuala ya nidhamu
No comments:
Post a Comment