LILE tamasha
kubwa la Muziki wa Injili Mkoani Mwanza Liitwalo Lakwetu Concert linatarajia
kufanyika kwa Kishindo Jijini humo tarehe 9 Juni Mwaka huu.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Meneja wa Famara Promotion waandaji wa Lakwetu Concert
Bi Catherine Mniko alisema kuwa tamasha la Mwaka huu litakuwa kubwa kutokana
Maandalizi yaliyofanywa na Kamati ya uratibu.
Catherine
alisema Kamati imejiandaa vya kutosha kuratibu kila kitu na wanaamini tamasha
la mwaka huu litakuwa kubwa tofauti ya miaka miwili iliyopita toka lianzishwe
Jijini Mwanza.
"Toka
Lakwetu Concert lianzishwe tumeona ukuaji mkubwa wa tamasha, watu wameanza
kutuelewa na kulipenda tamasha letu" alisema Bi Catherine.
"Mwaka
huu tumeanza Maandalizi mapema Sana toka mwezi wa pili na hadi kilele chake
tunaamini kusudi letu litakuwa limefikia hatua nzurii zaidi"
"Tumepita
kwenye makanisa Saba Jijini Mwanza kwa kuandaa matamasha ya kuimba kwa
kuzileta kwaya mbalimbali kutoka madhehebu yote, waimbaji wa bendi na waimbaji
binafsi kwa ajili ya kumsifu Mungu pamoja na kujiandaa na kilele Cha tamasha
letu la Grand Finale"
Bi Catherine
alisema tamasha la finali la Lakwetu Concert litakuwa na Mambo Mbalimbali
mazuri Sana kupita miaka miwili iliopita .
Alisema
tamasha hilo litafanyika Katika Uwanja wa CCM Kirumba tarehe 9 Juni Mwaka huu
kwa vikutanisha Vikundi zaidi ya arobaini kutoka Mikoa mbalimbali Nchini.
Pia
watakuwepo washiriki wa Shindano la Rock City Gospel Search 2019 siku hiyo na
watazamaji watapata nafasi ya kuwaona ili wawafahamu na kuviona vipaji
walivyonavyo.
Tamasha la
Lakwetu Concert ni Kongamano kubwa la Kuimba na kusifu lililobuniwa makusudi
kuwaleta waimbaji wa Muziki wa Injili pamoja ili kumsifu Mungu kwa Nyimbo na
tenzi, linalozunguka Mikoa mbalimbali Nchini.
No comments:
Post a Comment