NACTE YASITISHA UDAHILI KOZI YA HUDUMU YA AFYA NGAZI YA JAMII ( COMMUNITY HEALTH) KWA MWAKA WA MASOMO 2019/2020
Mkurugenzi wa uzingativu, ufuatiliaji na
tathmini wa (NACTE) Jofrey Oleke akizungumza na waandishi wa habari juu
ya kuanza udahili mpya kwa wanafunzi, katika maonyesho ya Elimu ya
Ufundi na Mafunzo Jijini Dodoma.
Mdahili wa wanafunzi kutoka Baraza la
Elimu ya Ufundi na Mafunzo(NACTE) Twaha A Twaha akitoa ufafanuzi wa
jambo flani kwa waandishi wa habari jijini Dodoma wakati wa mkutano na
wanahabari wakati wa kutangazwa kufunguliwa kwa udahili kwa mwaka
2019/2020.
………………
Na.Alex Mathais,Dodoma
Baraza la Taifa la Elimu ya
Ufundi(NACTE)limetangaza kusitisha udahili wa wanafunzi wapya wa
program ya Huduma ya Afya Ngazi ya Jamii(Community Health) kwa mwaka wa
masomo 2019/2020 hadi hapo itakapotangaza tena.
Akizungumza mbele ya wanahabari Jijini
Dodoma leo Mkurugenzi wa uzingativu, ufuatiliaji na Tathmini wa NACTE
Jofrey Oleke, amesema maombi ya udahili kwa waombaji wapya wa
Astashahada na Stashahada kwa mwaka wa masomo 2019/2020, umesitishwa
hadi hapo baraza litakapotangaza maamuzi mengine.
Kufutwa kwa udahili huo kumetokana na
maelekezo yaliyotolewa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee
na Watoto kwamba kwa mwaka huu wa masomo hakutakuwa na kozi hizo.
Kuhusu kusitishwa kwa udahili, amesema
baraza limepokea maagizo kutoka wizara ya afya ambao ndio wanaosimamia
kozi zote za afya, kuwa katika mwaka huu wa masoma hakutakuwa na udahili
katika ngazi hiyo afya ya jamii nasi tunatekeleza.
“Baraza linavitaarifu vyuo na umma
kwamba udahili wa wanafunzi katika programu ya Huduma ya afya Ngazi ya
Jamii umesitishwa hadi hapo itakapotangazwa tena”,amesema.
Pia baraza limetangaza kufunguliwa kwa
udahili mpya kwa ngazi za Astashahada na stashahada kwa kozi zote
isipokuwa kwa kozi za ualimu na utaendelea mpaka tarehe 2 mwezi wa
tisa mwaka huu kwa vyuo vyote vinavyotoa mafunzo katika ngazi hizo.
Amefafanua kuwa kwa waombaji wa programu
za Afya katika vyuo vya Serikali watatakiwa ama kuomba moja kwa moja
kupitia vyuoni ambapo vyuo vitasawasajili kupitia baraza la chuo au
wanaweza kuomba kupitia tovuti ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (www.nacte.go.tz) kubonyeza kwenye ‘apply online'(SAVS).
Kuhusu waombaji wa programu za Afya
kwenye vyuo visivyo vya Serikali na waombaji wa programu nyingine zote
wanatakiwa kuomba moja kwa moja kwenye vyuo husika.
“Hivyo vyuo vitapokea maombi na kufanya
uchaguzi wa wanafunzi wenye sifa na kisha wawasilishe NACTE majina ya
waliochaguliwa kwa ajili ya uhakiki kabla ya kuyatangaza, vyuo
vinaelekezwa kuzingatia utaratibu wa udahili kama ulivyotolewa na baraza
katika mwaka wa masomo 2019/2020,”amesema.
Amewataka wahitimu wote wa Elimu ya
Sekondari na vyuo wenye sifa za kujiunga na kozi za Astashahada na
Stashahada, kufanya maombi kwa umakini ili kuweza kupata nafasi ya
kujiunga programu wanazozipenda na ambazo wanatimiza vigezo/sifa za
kujiunga nazo kwa mwaka 2019/2020.
Pia baraza limewashauri waombaji na
wazazi kuhakikisha kuwa wanaomba kwenye vyuo vinavyokidhi ubora ambavyo
vimeorodheshwa kwenye kitabu cha mwongozo wa udahili kwa mwaka wa masomo
mwaka 2019/2020 .
ahaaa sawa tangazo limeeleweka kabisa. sasa je nini hatima ya wahitimu wa kozi hyo community health technician kuanzia wale wa first intake na second intake? natumain nitapata majibu kabisa.
ReplyDeleteTangazo limeeleweka ila tunaomba kueleweshwa kuhusu hatima ya kozi ya afya ya jamii na muendelezo wake ni UPI? Maana tumesoma alafu atujui nn hatima yake.
ReplyDeletethanks 4information
ReplyDeleteTunahitaji kujuwa mwendelezo wake unakuwa jeh,?
ReplyDeleteKama umemaliza CH na umeajiriwa au haujaajiriwa Tia namba tuyajenge 0659929907
ReplyDelete