Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akisisitiza jambo wakati akifungua kongamano la Kimataifa la kisayansi kuhusu matumizi na athari za viuatilifu kwa afya za binadamu na mazingira katika nchi za afrika kusini mwa jangwa la sahara litakalofanyika katika ukumbi wa TPRI, leo tarehe 28 Mei, 2019 Jijini Arusha.
Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akifatilia jambo wakati wa kongamano la Kimataifa la kisayansi kuhusu matumizi na athari za viuatilifu kwa afya za binadamu na mazingira katika nchi za afrika kusini mwa jangwa la sahara litakalofanyika katika ukumbi wa TPRI, leo tarehe 28 Mei, 2019 Jijini Arusha.
Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti na Udhibiti wa viuatilifu ukanda wa Kitropiki-TPRI Dkt Margaret Mollel wakifuatilia uwasilishaji wa mada kwenye kongamano la Kimataifa la kisayansi kuhusu matumizi na athari za viuatilifu kwa afya za binadamu na mazingira katika nchi za afrika kusini mwa jangwa la sahara litakalofanyika katika ukumbi wa TPRI, leo tarehe 28 Mei, 2019 Jijini Arusha.
Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano la Kimataifa la kisayansi kuhusu matumizi na athari za viuatilifu kwa afya za binadamu na mazingira katika nchi za afrika kusini mwa jangwa la sahara litakalofanyika katika ukumbi wa TPRI, leo tarehe 28 Mei, 2019 Jijini Arusha.
Na Mathias Canal, Wizara
ya Kilimo-Arusha 220919
Taasisi ya Utafiti na Udhibiti wa viuatilifu
ukanda wa Kitropiki-TPRI imekuwa kitovu cha kuunda mifumo
mizuri inayosimamia na kudhibiti Biashara ya Viuatilifu.
Zipo baadhi ya nchi za Afika kusini mwa Jangwa la sahara ambazo bado
hazijatengeneza mifumo mizuri ya Kisheria na sera za kusimamia biashara za
viuatilifu.
Naibu waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba ameyasema hayo leo tarehe 28 Mei,
2019 Jijini Arusha wakati akifungua kongamano la Kimataifa la kisayansi kuhusu
matumizi na athari za viuatilifu kwa afya za binadamu na mazingira katika nchi
za afrika kusini mwa jangwa la sahara litakalofanyika katika ukumbi wa TPRI.
Mhe Mgumba ameipongeza Taasisi hiyo ya TPRI kwa kushirikiana na wadau
wengine kwa kuandaa kongamano hilo Kwani ni sehemu ya kuwajengea uwezo wadau
mbalimbali ili waweze kuhakikisha kuwa Visumbufu (Pests) haviwi kikwazo katika
kutimiza azma ya serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais John Pombe
Magufuli ya kujenga Tanzania ya Viwanda na kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka
2025.
Alisema kuwa umuhimu wa viuatilifu katika kuzalisha mazao ni jambo la wazi
na muhimu katika nchi za Ukanda wa kusini mwa Afrika na maeneo mengine duniani
hivyo kongamano hilo litakuwa chachu na taswira chanya katika maendeleo ya
kilimo nchini.
Alisema matumizi ya viuatilifu kwa tafsiri ya wengi
ni kupata mazao mengi na hivyo mapato ya kutosha na kupata uhakika wa
chakula. “Suala la madhara ya viuatilifu
hivi kwa afya ya binadamu na uchafuzi wa mazingira wengi hawalipi kipaumbele na
hawaoni kwamba ni tatizo. Tatizo linakuwa kubwa zaidi pale ambapo wengi
wanatumia viuatilifu bila kuzingatia maelekezo ya watengenezaji” Alikaririwa
Mhe Hasunga
Kadhalika alisema, Visumbufu vya mazao husababisha upotevu
wa karibia ya nusu ya mazao katika Bara la Afrika na nchi
zinazoendelea hivyo Bara la Afrika likiwa linakusudia kuzalisha chakula cha
kutosha kwa ajili ya watu wake ambao wanaongezeka kwa kasi, hivyo ni lazima wakulima
watumie mbinu mbalimbali za kupambana na visumbufu vya mazao.
“Ingawa viuatilifu vimeleta mafanikio makubwa sana duniani katika kupambana
na visumbufu vya mazao, visumbufu vya mifugo na binadamu, pia vinasababisha
madhara kwa binadamu na mazingira kwa upande mwingine” Alikaririwa Mhe Mgumba
Aidha, alisisitiza kuwa katika Bara la Afrika tatizo ni kubwa zaidi kuliko
maeneo mengine duniani kutokana na uwepo wa matumizi ya viuatilifu hata vile
ambavyo vimepigwa marufuku maeneo mengine duniani hivyo kuhisiwa kusababisha
madhara kwa maelfu ya watu wengi.
Alisema kuwa matumizi ya viuatilifu au biashara zinazohusiana na viuatilifu
zinaweza kusababisha madhara ya kiafya kwa watumiaji wa viuatilifu au kwa jamii
na vile vile kusababisha uchafuzi wa mazingira pale ambapo viuatilifu
havijatumika kwa njia zilizo sahihi na salama.
Tanzania kuna sheria mbili zinazoongoza katika kusimamia na kudhibiti
matumizi sahihi na salama ya viuatilifu.
Sheria hizi ni sheria ya udhibiti wa
visumbufu vya mimea Namba 13 ya Mwaka 1997 (Plant Protection Act No. 13 of
1997) na kanuni zake za mwaka 1999. Na sheria ya TPRI (The TPRI Act. No. 18
of 1979).
Hata hivyo, Baadhi ya nchi za Kiafrika zinazotumia viuatilifu kwa wingi na zenye
sheria hafifu za kusimamia matumizi ya viuatilifu, madhara ya viuatilifu ni mengi sana kutokana
na usimamizi hafifu na pia kutokuwepo kwa huduma ya upimaji wa madhara ya
viuatilifu katika afya ya binadamu.
MWISHO
No comments:
Post a Comment