Sunday, May 19, 2019

MADIWANI MANISPAA YA IRINGA WAMPONGEZA SALIM ASAS KWA KUCHANGIA MAENDELEO YA MANISPAA HIYO

Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) manispaa ya Iringa Salvatory Ngerera akiwa na madiwani wa kata ya Nduli, Kitanzini Miomboni, Mshindo, Gangilonga, Mwangata, Ruaha, Kitwiru, Mkwawa, Kihesa na Kwakilosa kwa pamoja wamempongeza mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas kwa kusaidia kukuza maendeleo ya manispaa ya Iringa
 Naibu meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata kupitia chama cha mapinduzi CCM akihutubia wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Miomboni Kitanzini
 Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) manispaa ya Iringa Salvatory Ngerera akiwa na madiwani wa kata ya Nduli, Kitanzini Miomboni, Mshindo, Gangilonga, Mwangata, Ruaha, Kitwiru, Mkwawa, Kihesa na Kwakilosa wakifurahia jambo walipokuwa jukwani
 Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) manispaa ya Iringa Salvatory Ngerera akiwa namadiwani wa kata ya Nduli, Kitanzini Miomboni, Mshindo, Gangilonga, Mwangata, Ruaha, Kitwiru, Mkwawa, Kihesa na Kwakilosa 


NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
 
Madiwani wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa wampongeza mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas kuchangia maendeleo ya mkoa wa Iringa katika sekta ya afya,miundombinu na sekta ya uchumi.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Kitanzini, Naibu meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata alisema kuwa MNEC Salim Asas amekuwa akichangia maendeleo kwa vitendo tofauti na wanasiasa wengine wa upinzani.

“Jamani wanairinga mliopo hapa naomba niwaambie kuwa MNEC Salim Asas amekuwa ajitoa kweli kweli kuhakikisha anakuza kipato kwa wananchi wa manispaa ya Iringa na mkoa kwa ujumla hasa ukianzia kwa machinga hadi wafanyabiashara wengine wote anamchango mkubwa mno” alisema Lyata

Lyata alisema kuwa MNEC Asas amefanikisha ujenzi wa jengo la kufulia nguo za hospitali ya Frelimo,ujenzi wa chumba cha kuhifadhia damu,ujenzi wa hodi ya watoto njiti hiyo yote imefanyika katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa na  kachangia ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Nduli hayo ni baadhi tu.

“Hayo niliyoyasema hii leo ni machache tu ila MNEC huyu amefanya mambo mengi mazuri ya kimaendeleo katika mkoa wa Iringa hivyo ni lazima kumpongeza kwa kwa kuhudi zake anazozifanya kutoka moyoni kwake kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa mkoa wa Iringa” alisema Lyata

Nao madiwani wa kata ya Nduli,Kitanzini Miomboni,Mshindo,Gangilonga,Mwangata,Ruaha,Kitwiru,
Mkwawa,Kihesa na Kwakilosa kwa pamoja wamesema kuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas  amesaidia kufanya maendeleo kwenye kata hizo.

“Ukija kwenye kata zetu utakutana na mchango wa kimaendeleo unaotokana na mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa Iringa (MNEC) Salim Asas hivyo ni lazima sisi kama madiwani tuendelee kumpongeza Asas kwa kuwa na moyo wa kujitolea mamilioni ya pesa kwa kufanya shughuli za kimaendeleo” walisema madiwani hao 

Kwa upende wake mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) manispaa ya Iringa Salvatory Ngerera alisema kuwa wananchi wa mkoa wa Iringa wanapaswa kuwadharau viongozi wa kisiasa ambao wamekuwa wakimtolea maneno mabaya kwa MNEC huyo.

“Wananchi wa Manispaa ya Iringa mnajine wenyewe mambo mengi mazuri ambayo Salim Asas amekuwa akiyafanya hapa hivyo tunatakiwa kuendelea kuwapuuza wanasiasa wote ambao wanamsema vibaya MNEC huyo” alisema Ngerera

No comments:

Post a Comment