KAFULILA AELEZEKA MPANGOKAZI WA USAIDIZI WA KISHERIA UKAMILIKE HARAKA
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David
Kafulila akinukuu baadhi ya maoni ya wadau katika kikao cha wadau wa
msaada wa kisheria kwa Mikoa ya Nyanda za juu Kusini inayojumuisha mikoa
ya Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa na Songwe, kulia kwake ni Msajili wa
Mashirika na taasisi zinazotoa Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya
Katiba na Sheria Felista Joseph
……………………….
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David
Kafulila ameelekeza kuwa mpango kazi wa kuratibu taasisi na mashirika
yanayotoa msaada wa kisheria kwa wananchi ukamailike haraka ili wananchi
wapate huduma ya usaidizi wa kisheria kwa ufanisi.
Kafulila ametoa maelekezo hayo jana
wakati akifungua kikao cha wadau wa msaada wa kisheria kwa Mikoa ya
Nyanda za juu Kusini inayojumuisha mikoa ya Njombe, Iringa, Mbeya, Rukwa
na Songwe
“Watu wengi wamepoteza haki zao kwa
kutokujua sheria au kutokuwa na fedha za kumudu gharama za mawakili
lakini serikali imetengeneza utaratibu wa kuratibu taasisi ambazo
zinatoa msaada wa kisheria bila malipo ili wananchi wengi zaidi
wasiojiweza waweze kupata msaada wa kisheria na wasikose haki zao”,
amesema Kafulila.
Amesema kuwa mpango kazi wa kuziratibu
taasisi zinazotoa msaada wa kisheria uwe unapimika na hasa uwe na lengo
la kutoa elimu kwa wananchi ili wajue kuwa hata kama hawana fedha za
kugharimia mawakili wa kuwatetea ili wapate haki zao au hawana elimu juu
ya sheria mbalimbali, zipo taasisi ambazo zinatoa huduma hiyo bila
malipo.
Naye Msajili wa Mashirika na taasisi
zinazotoa Msaada wa Kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Felista
Joseph amesema kuwa elimu kwa umma itapewa kipaumbele katika mpango kazi
huo na ni jambo la msingi ili wananchi wafahamu uwepo wa taasisi hizo
“Katika wiki ya msaada wa kisheria
tunatoa elimu kwa wananchi kupitia vipeperushi, radio mbalimbali,
tunazungumza nao katika maeneo mbalimbali pia orodha ya taasisi hizo
huwekwa katika maeneo yote muhimu ili wananchi wajue kuna taasisi ambazo
hutoa msaada wa kisheria pale ambapo watakuwa na uhitaji”, amesema
Joseph.
Kwa upande wake Mratibu wa shirika la
Gender and Social Reform Steward Shiwuga amesema shirika lake limekuwa
likipata vikwazo katika kutoa msaada wa kisheria bila gharama yoyote na
pia baadhi ya watendaji wamekuwa hawatoi ushirikiano kwao.
“Wananchi wakisikia huduma ya msaada wa
kisheria tunaitoa bure wengine haamini wamezoa kutozwa fedha lakini pia
baadhi ya watendaji wamekuwa hawatoi ushirikiano kwetu lakini
tunaendelea kuwaelimisha wananchi na watendaji na matokeo tunayaona kwa
sasa angalau ushirikiano umeanza kuongezeka na wananchi wanakuja kupata
msaada”, amesema Shiwuga.
Msajili Msaidizi wa Taasisi za Msaada wa
kisheria kwa Wilaya ya Ileje Rodrick Sengela ameeleza kuwa hapo awali
taasisi hizo zilijiendesha bila kuratibiwa pia baadhi ya watu wasio
waaminifu walikuwa wakiwarubuni wananchi na kuwatoza fedha nyingi pale
wanapohitaji msaada wa kisheria lakini kwa sasa wananchi wataelimisha
mahali sahihi pa kupata msaada wa kisheria bila malipo.
No comments:
Post a Comment