Friday, February 1, 2019

UVCCM WILAYA YA SERENGETI YAADHIMISHA KUZALIWA KWA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO





Umoja wa vijana wa ccm wilaya ya Serengeti (uvccm), wakiongozwa na katibu wa uvccm wilaya Serengeti ndg, Alphonce Patrick Muyinga (Black) Pamoja na Mjumbe wa kamati ya utekelezaji ( W ) Ndg, Muhochi   Leo Pamoja na vijana wilaya ya Serengeti kata ya Mbalimbali kwa kushirikiana na diwani wa kata hiyo Mh.John Ng'oina wameazimisha sherehe za kuzaliwa ccm kwa kukagua miradi katika kata hiyo ya Mbalimbali.

Pamoja na kusikiliza kero za wana nchi katika kata hiyo. pia diwani wa kata hiyo kwa niaba ya wana nchi alieleza kero ya maji katika kijiji hicho Ambacho Kuna mradi uliopaswa kukamilika mwaka Jana mwenzi wa 6 lakini mpaka Sasa unasuasua na kero ya maji imezidi  Kua kubwa hasa kwa vijiji vya kata hiyo.

Pia  Mh.Diwani huyo ameeleza juu ya kata yake yenye vijiji vitano Kua na kituo cha afya  kimoja, mpka Sasa ametafuta wahisani wa kusaidia huduma hiyo. wamejitokeza lakini changamoto ni nyingi katika wizara ya afya wanazokutana nazo.

Pia, Umoja wa vijana wa ccm wilaya ya Serengeti waliongea na vijana kuhusu elimu ya mikopo inayotolewa na serikali kwa vijana. Na kuwa kumbusha vijana wa kiume kuwaepusha mabinti na swala  la tohara. Kwa maana ni unyanyasaji kwa watoto wa kike.

Pia, Mabinti wawe jasiri kwa kutoa taarifa kwenye vyombo vya  ulinzi na usalama pale wanapo lazimishwa kufanya tohara.

Vilevile,Umoja wa vijana ccm wilaya ya Serengeti uliwakumbusha vijana kuwa, jukumu la kulinda amani ya nchi yetu ni la kila mtanzania.

Na Kuwaonya Kua vijana tusikubali kutumika kwa maslahi ya mtu binafsi. Pia tuwe mstali wa mbele kusema mazuri yanayo tendwa na serikali yetu. Lakini tusiwafumbie macho viongozi Bila kujali ni viongozi wa kisiasa au serikali Hata Kama wanatokana na ccm, Kama dhamira yao sio nzuri kwa masilahi ya taifa na ccm

No comments:

Post a Comment