Saturday, February 16, 2019

NAIBU WAZIRI JUMA AWESO AMETOA WIKI TATU KWA MKANDARASI KUKAMILISHA MRADI WA MAJI WA SAWALA

Naibu waziri wa maji Juma Aweso ametoa wiki tatu kwa kampuni ya mavonoa’s kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa Sawala uliopo jimbo la Mufindi kusini katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
NAIBU waziri wa maji Juma Aweso akimbana mkandarasi wa kampuni ya mavonoa’s kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa Sawala uliopo jimbo la Mufindi kusini katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.


NAIBU waziri wa maji Juma Aweso ametoa wiki tatu kwa kampuni ya mavonoa’s kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa Sawala uliopo jimbo la Mufindi kusini katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
Akizungumza mbele ya wananchi,wabunge na wafanyakazi wa halmashuri hiyo,waziri Aweso alisema kuwa amekuwa akipokea malalamiko mengi ya mkandasi huyo ambaye amekuwa hana mahusiano mazuri na viongozi wa halmashauri hiyo.
“Mimi niseme ukweli nakupa wiki tatu kuhakikisha unamalizia ujenzi wa mradi wa maji wa Sawala la sivyo utaniona mbaya na mimi ni mkali kweli kwa wakandasi wamepewa kazi na serikali na wanashindwa kutekeleza mradi kama ambavyo mkabata ulisema hivyo nakupa wiki tatu kuhakikisha wananchi wanapata maji” alisema Aweso
Aweso alisema serikalia ya awamu ya tano haita kubari kumuanda mkandarasi yeyote Yule aliyepewa kazi na serikali anashindwa kukamilisha mradi wakati fedha amepewa,mkandarasi huyo atachukuliwa hatua za kisheria haraka sana kwa kuwa saizi hakuna mtu kutumia vibaya pesa za serikali kama ilivyokuwa huko nyuma.
“Walizoea kuzichezea pesa za serikali miaka ya huko nyuma kwa sasa hakuna mkandarasi tayeweza kuichezea serikali ya awamu hii kwa kuwa sisi wateule wa Rais wetu Dr John Pombe Magufuli hakuna anayekubari kutumbuliwa kisa wakandarasi kufanya vibaya kwenye miradi waliyopewa” alisema Aweso
Aidha naibu waziri Aweso aliwatoa hofu viongozi wa halmashuri ya wilaya ya Mufindi kuhusu mkandarasi huyo kuwa akishindwa kutekeleza mradi huo ndani ya wiki tatu hizo basi sheria itachukua mkoando wake.
“Mkuu wa wilaya,mbunge,mkurugenzi na mwenyekiti wa halmashauri niwahakikishieni kuwa nitatakuja tena tarehe mbili mwezi wa tatu hapa kuja kuangalia kuwa huu mradi umefikiwa wapi na makubariano yetu ameyatekeleza mkandarasi huyu” alisema Aweso
Awali mkuu wa wilaya ya Mufundi Jamhuri William alimueleza naibu waziri kuwa mkandarasi huyoamekuwa anaidharau serikali kwa kuwa mara kwa mara ameandikiwa barua na serikali ya wilaya lakini hajawahi kujibu hata mara moja kitendo kinachoashiria dharau.
“Huyo mkandarasi amekuwa anatusumbua sana maana tunamuita mara kwa mara hataki kuitika wito wetu hivyo hizo ndio dharau kubwa kiasi kwamba anashindwa hata kuendelea kutekeleza mradi huu ambao wananchi wanategemea kuwa mkombozi wao” alisema Jamhuri William
Mkuu wa wilaya alisema kuwa atamkamata na kuwa ndani mkandarasi huyo kwa kuwa anachelewesha kuteleza mradi huo wa maji na kusababisha wananchi kuichukia serikali kwa kusema kuwa wametoa ahdi hewa kitua ambacho sio kweli.
“Mheshimiwa naibu waziri hapa Sawala tunashindwa hata kufanya mikutano ya hadhara kwa ajili ya huu mradi wa maji ambao mwazoni wananchi walijenga imani kubwa wakati wa kusainiana mkataba wa kutekeleza mradi huu” alisema Jamhuri William
Akitoa malalamiko hayo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi Festo Mgina alimwambia naibu waziri wa maji Juma Aweso kuwa hamhitaji tena huyo mkandarasi kwa kuwa amekuwa kikwazo cha kuleta maendeleo ya wananchi kwa kushindwa kutekeleza mradi huo wa maji.
“Huyu kwetu ni kero kubwa mno mheshimiwa naibu waziri wa maji,sisi kama halmashauri hatupo tayari kufanya kazitena na huyu mkandari kwa ujeuri wake na kushindwa kuiheshimu sekali ya wilaya kwa kushindwa kumtua ndo mwanamke” alisema
Nao baadhi ya wananchi walijitokeza hapo walimwambia naibu waziri kuwa mkandarasi huyo hafanyi kazi ipasavyo kwa kuwa amesikia waziri unakuja ndio na yeye ameanza kazi jana tu ya kukarabati tenki hili la maji ili ukifika uone kama yupo anafanya kazi wakati sio kweli.
Hata hivyo naibu waziri Juma Aweso alimalizia kwa kusema kuwa ifikapo tarehe mbili mwezi wa tatu mradi huo uwe umekamilika na wananchi waweze kupata maji na kufanikisha adhima ya Rais ya kumtua ndoo mwanamke.

No comments:

Post a Comment