Saturday, February 9, 2019

MHE HASUNGA KUONGOZA MKUTANO WA SEKTA NDOGO YA MAZAO NA SEKTA BINAFSI


Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (Mb)

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe anapenda kuwataarifu Wakuu wa Taasisi za Utafiti katika Sekta ya Kilimo pamoja Watendaji Wakuu wa Sekta Ndogo ya Mazao ya Kilimo na Sekta Binafsi kwamba, kutakuwa na Mkutano Maalum baina ya Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (Mb) na Wadau hao utakaofanyika tarehe 11 Februari 2019 (kwa watafiti) na tarehe 12 Februari 2019 (sekta binafsi) kuanzia saa 4:00 asubuhi.

Mkutano huo utafanyika katika Ukumbi wa Kilimo I, Wizara ya Kilimo, Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Kilimo atatumia Mikutano hiyo kubadilishana uzoefu pamoja na kujadili mambo mbalimbali kuhusiana na maendeleo ya Sekta ya Kilimo. Aidha, atapenda kufahamu mchango wa kila Taasisi na wadau wa sekta binafsi katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za kilimo ikiwa ni pamoja na Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) pamoja na changamoto zilizopo na utatuzi wake.

Imetolewa na:-
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Kilimo
DODOMA

3 comments:

  1. Huu mkutano wa watafiti utahusu waliopo serikalini tu au wote?

    Huu wa sekta binafsi (Feb12) una watu maalum au yeyote anaweza kuhudhuria?

    ReplyDelete
  2. Nimuhimu sana kushiriki. Ngoja tufuatilie ikiwa naweza kushiriki mkutano huu muhimu.

    ReplyDelete