Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama ameiagiza Tume ya Usuluhishi na Uamuzi, kuweka mpango Maalum wa kuhakikisha migogoro katika sekta binafsi ya Ulinzi haizalishwi tena kwa wingi kwani inasababisha kutumika vibaya kwa rasilimali muda kati ya mwajiri na Mfanyakazi hali inayopelekea kuchelewesha Maendeleo.
Waziri Mhagama amebainisha sekta nyingine zinazoongoza kuwa na migogoro mahala pa kazi kuwa ni Sekta ya Ujenzi na Sekta ya Elimu. Aidha, ameitaka Tume hiyo kufanya utafiti kwa sekta zote zinazoongoza kwa migogoro ya kikazi ili kubaini chanzo cha migogoro hiyo na kuandaa Mkakati Maalum wa kuishughulikia.
Mhagama ameyasema hayo leo mjini Morogoro tarehe 14
Januari, 2019, wakati wa kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Tume ya
Usuluhishi na Uamuzi kilichowakutanisha Wasuluhishi na waamuzi wa migogoro
ya kikazi nchi nzima.
"Hii sekta Binafsi ya Ulinzi kwa nini
huko migogoro haiishi? Nataka mpango wa kumaliza migogoro hiyo, shirikianane
na Taasisi nyingine muweke mpango maalum utakao weza kutatua na kuhakikisha
haizalishwi mogogoro mingine" Alisisitiza Mhagama.
Mhagama alifafanua kuwa Serikali ya Awam ya Tano
inayoogozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiriakwa vitendo vya kupiga
vita uzembe, ubadhirifu na vitendo vyote Vya rushwa mahala pa
kazi.
"Nisisitize kazi ya Usuluhishi na
Uamuzi ni kazi ya heshima na pia ni kazi ya wito. Hivyo wekeni
mkazo kwenye suala la Usuluhishi ili kupunguza muda na mlundikano
wa mashauri, pia bainisheni sekta nyingine zenye migogoro
mikubwa. Elimu ni vyema iendelee kutolewa kwa Wadau kuhusu Sheria za
Ajira na mahusiano kazini." alieleza
Mhagama.
Awali akiongea katika Mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi, Shanes Nungu alibainisha kuwa Tume hiyo itatekeleza maagizo hayo kwa kuboresha Mkakati Wa Mpango kazi Wa Tume ili kuwa na mpango mkakati kwenye mtazamo Wa kupunguza migogoro na unaolenga kumaliza migogoro kwa nataka katika sekta zinazoongoza kuwa na migogoro mahala pa kazi.

"Tumekuwa
tunajitahidi kumaliza na kuipunguza migogoro ya kikazi, kwani tumefanikiwa
kumaliza migogoro hiyo kwa asilimia 80 kwenye hatua ya Uamuzi na asilimia 77,
kwenye hatua ya Usuluhishi" alieleza Nungu.
Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ambapo Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Tume hiyo kimefanyika kwa mujibu wa Agizo la Rais Na.1 la mwaka 1970. Baraza hilo huiwezesha Tume kuboresha Huduma na masuala ya utatuzi Wa migogoro ya kikazi kwa njia ya Usuluhishi na Uamuzi.

No comments:
Post a Comment