Dkt Iveta Gobovska kutoka Chuo Kikuu cha Ltvia akizungumza jambo katika hafla maalumu ya kupokelewa na kuanza kwa mafunzo ya kuwapatia wagonjwa dawa za usingizi kwa njia ya kisasa (Regional block anaesthesia) hifla hiyo imefanyika leo katika Taaisisi ya MOI
Katibu mkuu wa chama cha mabadkari bingwa wa Usingizi Tanzania SATA Dkt Albert Ulimali akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kuwapokea wakufunzi wa kutoa dawa usingizi kutoka nchini Latvia katika ukumbi mpya wa mikutano wa MOI
NA ANDREW CHALE
TAASISI ya tiba ya Mifupa MOI
imeanzisha huduma ya kutoa dawa za usingizi (Reginal block Anaesthesia) ambapo
eneo husika linalofanyiwa upasuaji ndilo litakolo husika kwa kuzuia mishipa ya
fahamu na hivyo mgonjwa kuwa macho na kuzungumza au hata kusoma gazeti
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface katika hafla ya kuwapokea wakufunzi
wawili kutoka Chuo kikuu cha Latvia cha nchini Latvia ambao watatoa mafunzo
hayo ya kibingwa ya kuzuia mishipa ya fahamu katika eneo linalofanyiwa upasuaji
badala ya kumlaza mgonjwa usingizi (Nusu kaputi) kwa zaidi ya siku kumi kwa
madaktari bingwa wa MOI na madaktari walio mafunzoni
“Huu ni muendelezo wa mafunzo ambayo
tulishayaanzisha kwa mdakatari wetu , lengo kubwa la mafunzo haya na ujio wa
wakufunzi hawa ni kuhakikisha huduma hii inaendlea kutolewa hapa MOI. Ni mbinu
bora na salama ya kumlaza mgonjwa kwaajili ya upasuaji ambapo mgonjwa anaweza
kufanyiwa upasuaji huku anasoma kitabu (Novel) ambapo baada ya upasuaji mgonjwa
hapati maumivu makali na anaweza kuruhusiwa kwenda nyumbani siku hiyohiyo”
Alisema Dkt Boniface
Dkt Boniface amesema pamoja na
wakufunzi hawa kutoa mafunzo , Taasisi ya MOI itasiani mkataba wa ushirikiano
na Chuo Kikuu cha Latvia lengo kuu ikiwa ni kubadilishana uzoefu katika utoaji
wa huduma za kibingwa za Usingizi (Anaesthesia)
“Kwa kuanza tutasaini mkataba wa
ushirikiano wa miaka mitatu ambapo watalaamu kutoka hapa watapata fursa ya
kujifunza kwenye Chuo chao lakini pia watakuja hapa kutoa mafunzo ya muda mfupi
kama ambavyo hawa wamekuja” Alisema Dkt Boniface
Dkt Boniface ameongeza kwamba kwa
sasa Taasisi ya MOI imeanzisha huduma ya kulazwa na kufanyiwa upasuaji siku
hiyohiyo yaani (Same day Surgery) hivyo huduma hii itatumika katika wagonjwa
wanaofanyiwa upasuaji na kuruhusiwa kwani wagonjwa hawapati maumivu makali
baada ya upasuaji na hakuna masharti magumu baada kufanyiwa upasuaji
Kwa upande wake Profesa Alex Miscuks
kutoka Chuo Kikuu cha Latvia amesema ni heshma kubwa kupata fursa ya kuja
kubadilishana uzoefu hapa Tanzania kwani pamoja na kutoa mafunzo atapata fursa
ya kujifunza mambo mengi.
“Nashukuru sana kwa kunialika,
nimefurahi kukutana na madaktari wazuri na wazoefu hapa MOI, naamimi mimi pia
nitajifunza mambo mengi kwenu, ahsnteni sana” alisema Prof Miscuks
Kwa upande wake Dkt Iveta Gobovska
ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha wagonja mahututi katika hospitali ya Chuo
Kikuu cha Latvia amesema amefarijika kupata fursa ya kuja kubadilishana uzoefu
na madaktari wa Tanzania na anamini pande zote mbili zitanufaika na mafunzo
haya.
Mwisho
No comments:
Post a Comment