Sunday, January 6, 2019

VIJANA WATAKIWA KUPUUZA MANENO OVU KWA WASIOYATAKIA MEMA MAPINDUZI YA ZANZIBAR




Na Ishraa Seif Ali-Zanzibar
Naibu   waziri wa vijana utamaduni sanaa  na michezo   Zanzibar  Lulu Msham Abdallah  amewataka  vijana  kuachana  na  maneno  mabaya  yanayosemwa  na    baadhi   ya   wanajamii   wasiotakia   mema mapinduzi   matukufu  ya Zanzibar  na badala yake  kuyaenzi na kuyalinda mapinduzi   hayo  .
Akifungua  kongamano la Vijana na Uzalendo kuelekea kilele cha maadhimisho ya kusheherekea miaka 55 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964  huko  katika ukumbi wa karibu  mjini  unguja.
Amesema  kuwa   wazee   walijitolea muhanga  kwa ajili ya kuleta uhuru  ambao leo  umeweza  kuleta maendeleo makubwa ndani ya jamii ikiwemo  suala la elimu  bure  na   matibabu   bure.
Aidha  naibu  huyo  amewasisitiza vijana  hao  vijana kuachana na vitendo vinavyokinzana na maadili yetu vikihusisha matumizi ya madawa ya kulevya, maambukizi ya ukimwi, ukatili na udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
Akitoa  mada  ya miaka  55  ya mapinduzi   matukufu  ya Zanzibar    mkuu  wa mkoa  mjini magharibi  mh ayoub  mohammed  mahmoud  amesema kuwa   ili  kuyaenzi  mapinduzi  basi ni vyema   kwa wannanchi kusoma kwa bidii  ,kufanya kazi  kwa bidii  na kuwa  na uzalendo  wan chi yao  .
Baadhi   ya   vijana walioshiriki   katika   kongamano  hilo  wamesema kuwa  kongamano hilo  limeweza kuwakuza kiakili na kuahidi kuyatunza mapinduzi  hayo  na kudumisha amnai na utulivu  wan chi   
Katika ongamano hilo  mada nne zimejadiliwa  ikiwemo Historia ya Zanzibar kabla ya Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964, mchango wa Mapinduzi katika maendeleo ya Zanzibar, nafasi ya vijana katika kuyaenzi na kuyalinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na Mapinduzi matukufu ya Zanzibar yanavyojenga uzalendo kwa vijana.   

No comments:

Post a Comment