Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso Akielekea kukagua tanki la Maji katika mradi wa Igogwe katika Manispaa ya Ilemela wakati wa ziara yake ya siku moja kukagua miradi ya maji mkoani Mwanza. Wa pili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Wazari wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula.
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso (wa pili kushoto) akiangalia ujenzi wa mradi wa maji katika kata ya Bugogwa Manispaa ya Ilemela wakati wa ziara yake ya siku moja kukagua miradi ya maji mkoani Mwanza. Wa tatu kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akipanda katika Tanki la maji kujionea ujenzi wa tanko hilo wakati Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso alipokagua miradi ya maji katika jimbo la Ilemela mkoani Mwanza.
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wanaojenga tanki la maji katika mradi wa maji vijijini eneo la Igogwe Manispaa ya Ilemela Mwanza wakati wa ziara yake ya siku moja kukagua miradi ya maji mkoani Mwanza. (PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA)
Na Munir Shemweta, ILEMELA
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso ametembelea miradi ya Maji katika
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Ilemela
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa jitihada
za kuwapatia wananchi wa jimbo hilo huduma ya maji safi na salama.
Katika ziara hiyo Aweso alijionea changamoto mbalimbali
zinazoikabili miradi ya maji katika manispaa hiyo pamoja na kero ya maji
wanayoipata wananchi wa Kata ya Bugogwa yenye mitaa kumi na tano na wakazi
wapatao 32,000 ambao kwa muda mrefu hawana huduma ya maji licha ya juhudi za
mbunge wa jimbo la Ilemela Dk Mabula kuwachimbia visima.
Mbunge wa Jimbo hilo Dk Mabula ameiomba Wizara ya Maji kuwapatia
wananchi wa kata ya Bugogwa huduma ya maji katika mradi wa maji vijijini kutokana
na chanzo cha maji cha mradi huo kupitia eneo lao.
Kwa Mujibu wa Dk Mabula, pamoja na chanzo cha mradi wa maji
vijijini kuwa katika kata ya Bugogwa jimboni humo lakini wananchi wake
hawajajumuishwa kwenye mradi jambo linaloleta sintofahamu kwa wakazi hao ambao
sasa wanaona kutengwa na serikali jambo alilolieleza kuwa linaweza
hata kutishia usalama wa mradi.
Alisema, njia pekee ya kuwafanya wananchi wa kata ya Bugogwa
kufurahia matunda ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli ni
kuwapatia huduma ya maji safi na salama kitendo kinachotafsiriwa kama kumtua
ndoo mama kichwani.
Kufuatia ombi hilo, Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso alimuagiza
Mhandisi wa Maji katika Manispaa ya Ilemela Anna Mawala pamoja na Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Mwanza (MWAUWASA) Injinia Anthony
Sanga kushirikiana kuandaa mpango mdogo utakaowezesha wakazi wa kata
nao kufaidika na mradi na mapendekezo hayo yawasilishwe wizarani mapema ili
kufanyiwa kazi.
Aweso alisema kuwa, Wizara ya Maji haiwezi kuwa kikwazo kwa
wananchi kupata huduma ya maji kwa kuwa huduma hiyo haina mbadala hivyo
Serikali itafanya kila jitihada kuhakikisha wananchi hao wanapata huduma ya
maji safi na salama ili kuondokana na kero ya muda mrefu.
Mtendaji wa Kata ya Bugogwa Manispaa ya Ilemelea mkoa wa Mwanza
Rashid Sukwa alisema kata yake imekuwa na tatizo la maji kwa muda mrefu pamoja
na juhudi za mbunge wa jimbo hilo Dk Mabula kusaidia kuchimba visima lakini
baadhi ya wananchi wanatumia visima vya asili.
Ameitaja baadhi ya mitaa yenye changamoto kubwa ya maji katika
kata hiyo kuwa ni pamoja na Lugezi, Igombe A na B, Bugogwa, Kigote, Bugigwa,
Kabaganja, Kasamwa, Kayenza Ndogo, Kisonde, Kilabela, Isanzo, Igogwe pamoja na
Nkoronto.
Mmoja wa wakazi wa Bugogwa Janet Lusia alimshukuru Naibu Waziri wa
Maji Jumaa Aweso kwa kuona umuhimu wa wananchi wa kata hiyo nao kufikiriwa
kupata maji katika mradi huo kwa kuwa wametaabika kwa muda mrefu pamoja na
jitihada za mbunge wao kuwachimbia visima.
------------------------------ ------MWISHO------------------ ------------------------------ --------------
MAELEZ YA PICHA
PIX NO 1- Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso Akielekea kukagua tanki
la Maji katika mradi wa Igogwe katika Manispaa ya Ilemela wakati wa ziara yake
ya siku moja kukagua miradi ya maji mkoani Mwanza. Wa pili kulia ni Mbunge wa
Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Wazari wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk
Angeline Mabula.
PIX NO 2- Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso (wa tatu kushoto)
akimsikiliza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mijini mkoani Mwanza Injinia Anthony
Sanga wakati wa wakati wa ziara yake ya siku moja kukagua miradi ya maji mkoani
Mwanza. Wa pili kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula.
PIX NO 3- Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso (wa pili kulia )
akimsikiliza Mhandisi wa Maji katika Manispaa ya Ilemela Anna Mawala wa wakati
wa ziara yake ya siku moja kukagua miradi ya maji mkoani Mwanza. Wa pili
kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula.
PIX NO 4- Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso (wa pili kushoto)
akiangalia ujenzi wa mradi wa maji katika kata ya Bugogwa Manispaa ya Ilemela
wakati wa ziara yake ya siku moja kukagua miradi ya maji mkoani Mwanza. Wa tatu
kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula.
PIX NO 5- Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akizungumza baada ya Naibu
Waziri wa Maji Jumaa Aweso kukagua miradi ya maji katika jimbo la Ilemela
mkoani Mwanza.
PIX NO 6- Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline Mabula akipanda katika Tanki la maji
kujionea ujenzi wa tanko hilo wakati Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso
alipokagua miradi ya maji katika jimbo la Ilemela mkoani Mwanza.
PIX NO 7- Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso na Mbunge wa Jimbo la
Ilemela ambaye pia ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angeline
Mabula wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wanaojenga tanki la maji
katika mradi wa maji vijijini eneo la Igogwe Manispaa ya Ilemela Mwanza wakati
wa ziara yake ya siku moja kukagua miradi ya maji mkoani Mwanza. (PICHA
ZOTE NA MUNIR SHEMWETA)
No comments:
Post a Comment