Thursday, January 24, 2019

MNEC MWAKITINYA AMSHUKIA TUNDU LISSU ASEMA IKUNGI WALIMCHAGUA KUWATUMIKIA SIO ZIARA ZA ULAYA KUITUKANA NCHI YAKE



Ikumbukwe siongei kwa niaba ya Taasisi Fulani bali naongea kama MNEC. Napenda kumpongeza Rais wangu Dr. John Pombe Joseph magufuli kwa uchapakazi wake anaouonesha siku hadi siku kwani katika kipindi kifupi Mh. Rais amejipambanua kutatua shida za wananchi, tumeshuhudia miundo mbinu inayojengwa siku hadi siku, ufufuaji wa shirika la ndege Tanzania (ATCL), anajenga hospitali, ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), ujenzi wa barabara za juu na wapo watu wanaosema maendeleo ya watu kwanza ila niwaambie hakuna maendeleo ya watu pasipo maendeleo ya vitu nikimnukuu Rashid NM, and Ngalawa F 2016 katika kulinganisha kwao logistic industry ya Tanzania na turkey walisema kukua kwa miundombinu ya Tanzania na sekta ya usafiri ni msingi kwa maendeleo ya Taifa.

Sasa watu wasiongee bila ya kusoma tusiwapoteze watanzania katika ramani ya kumtia Moyo Rais wetu kipenz Dr. magufuli na niwaambie sitawavumilia tena kuzungumza uongo wenu, kejeli zenu na mipasho yenu.

Tumuunge mkono Rais wetu, uzalendo hauna bei mimi namfananisha huyu mzalendo magufuli kama Mussa katika biblia maana Mussa alipopewa kazi na Mungu aliifanya kwa moyo wote huku akilaumiwa na wana wa Israel waliokuwa wakitolewa misri kwenda kanani, niseme tu Rais Magufuli ndio mtu sahihi wa kutupeleka katika nchi yenye maziwa na asali na Tanzania yenye neema inakuja na imeshaanza kuja, tunapobadilika kutoka sehemu tuliyozoea kuja mpya lazima tuumie kidogo ila tunaumia kwa manufaa ya taifa, kwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo, mimi sitokuwa tayari watoto wangu kufukua mifupa yangu siku nakuwa marehemu na kusema baba wewe ulikuwa wapi kutomtetea Rais magufuli wakati anatukanwa, siko tayari kupigwa viboko na wanangu siku ninapokuwa siko hapa duniani. TUMUUNGE MKONO

1. Niwashukuru mahakama kuu kutupilia mbali shauri batili la muungano wa vyama vya siasa uchwara, hawa wanaojiita wapinzani lakin kiuhalisia sio wapinzani wenye tija, wanaupinga sana huu muswada na kusema unampa mamlaka makubwa msajili wa vyama vya kisiasa mimi nauona muswada huu hauna shida kabisa na wao wanaukataa sababu unawabana juu ya pesa za uma walizozoea kuzitumbua, pesa zilikuwa zikitumika kiholela sasa msajilli atakuwa na jicho la karibu hili ndio linalowafanya waukatae muswada ila wanatumia sababu zingine zisizo na tija, zito na wenzake wanalia wakijua biashara zao za kuzitafuna hizi pesa kihasara hasara ndio mwisho wake.

Shauri walilolipeleka linakiuka kifungu 8 (2) cha sharia za haki za msingi na wajibu sababu hawakufuata taratibu ‘mtu yoyote anayedai haki zake zinakiukwa ama zinaelekea kukiukwa anapaswa kutafuta nafuu kwa kutumia njia nyingine zilizopo kwanza kabla ya mahakamani’ sasa zito kama kawaida yake moja kwa moja akakimbilia mahakamani kutafuta huruma ya wananchi kupitia vyombo vya habari, alidhani ataiyumbisha mahakama yetu, ila nawapongeza muhimili huu muhimu wa sheria kwa hili jambo kwani wamefanya jambo zito sana na zuri niwaombe mahakama kufanya kazi kwa misingi na taratibu za kisheria.

2. Nimpongeze CAG kwa kuitikia wito wa bunge kwani kauonesha ukomavu mkubwa na wenye tija kweli kupita maelezo sasa zito aache kufuatilia mambo yasiyomuhusu asiwe ni mtu anayefanya siasa za matukio kama ameshindwa siasa arudi nyumban na nimhakikishie zitoo mwaka 2020 harudi bungeni, kwa mfano hili jambo la CAG aliiomba mahakama imlinde CAG sasa mimi nizishauri mamlaka zote na vyombo vyote kuwa yoyote yule bila kujali nyadhifa yake akienda popote na kutukana taasis yoyote kama taifa wasimvumilie na kama ningekuwa na mamlaka ningeanza na huyu Lissu anavyoropokaropoka huko nje ya nchi, ningepambana nae kisawasawa.

3. Zitto Amani tuliyonayo Tanzania ni kubwa sana na watanzania tumekuwa tukifurahia hii amani tuliyonayo sasa tabia yako ya kujifungia chumbani na kutunga unataka kuuliwa tabia hiyo ikome mara moja, maana imekuwa ni kawaida yako kuvibuni hivi vitu, usalama wa taifa wanapambana kuhakikisha taifa tuko salama katika kila Nyanja, kazi wanayofanya ni nzuri nakuomba uache kutengeneza hofu katika akili za watu unasema umetishiwa kuuwawa sisi tutajuaje kama umetishiwa ama umetunga tupe ushahidi tujihakikishie na nikukumbushe bungeni palikuwa na wananchi wa kawaida wengi tu wakulima, wafanya biashara kama aliyekuambia hivyo alikuwa mwananchi wa kawaida tena mwananchi wako wa kigoma kukuambia dawa yako ni kukuua maana hauna tija katika jimbo lako sisi tutajuaje? Lakini kuua haina maana moja ipo maana nyingine ya mtu kuuliwa kisiasa yani kumalizwa hivyo nenda tumikia wananchi wako nina uhakika kama uliambiwa vile basi yamkini ni mwananchi wako wa kigoma ila bungeni hawakuwa ma afisa usalama tu bali walikuwa watu mchanganyiko mchanganyiko kutokana na shuguli yenyewe ya kupokea maoni.

4. Huu muswada wa vyama vya siasa upo mpango mkakati wa baadhi ya mabeberu ambao wamewekeza katika pesa zao kuhakikisha wabunge wanashawishiwa kutoupitisha mimi niwaambie taarifa zenu zipo, account mlizoanza kuingiziwa hizo fedha tunazijua. Hivi hamuwezi kufanya mambo bila kuwategemea hao mabeberu? wanataka nini na Tanzania kwanini hawafanyi haya mambo kwao niwakumbushe tu hakuna anayetoa pesa akiwa hana malengo na pesa yake hizo pesa mtagawana ila adhma yenu mbovu itashindwa na huo ndio ukweli. Nia njema itashinda daima na nia ya huu mswada ni njema huu muswada utakuwa sheria hakuna namna.

5. Tundu Lisu Tundu Lisu Tundu Lisu nimekuita mara tatu nataka nikuambie wanasingida hawajakuchagua ufanye ziara katika nchi za wenye nia mbaya na Tanzania, filamu mnazotuchezea zimekosa weledi kwa waandishi walioandika script hizo, nikuambie tu huko uliko hautafaidika na lolote ni vyema utambue Tanzania ni nchi huru tulishakombolewa kutoka kwa mkoloni sasa tumebaki kujikomboa kiuchumi kama taifa, umekosa uzalendo na utaifa na kuamua kuitukana ardhi inayojua shida zako zote na ardhi utakayozikwa siku ukifa, mwanaume hatukani katika nchi anazofadhiliwa, kama wewe kidume rudi Tanzania na utukane ukiwa Tanzania hapo ndipo tutajua wewe ni mwanaume wa shoka, nikuase uache tamaa na unayoendelea nayo katika nchi za watu, usitutusi kwa haki za binadamu na demokrasia angali wewe unao uhuru wa kututukana pindi ukija Tanzania, sasa nimepigiwa simu na wananchi wako wanataka nikawe mbunge wao sasa nikuambie tu endapo ukichelewa nakuhakikishia nitakuwa mbunge.

Wako mtiifu
MUSSA MWAKITINYA – MNEC

3 comments:

  1. Tunahitaji wabunge wenye uelewa mkubwa wa jamii ya Tanzania ukoje na inahitaji nini. Tanzania hatuhitaji aina ya demokrasia ambayo inahubiriwa duniani kote lakini hata mwanzilishi wake haifuati ipasavyo. Tanzania tunahitaji Uchumi wetu uwe wa kati, elimu iboreshwe, miundombinu iimarishwe ili hata bibi yangu kule kwimba mwanza aone manufaa yake. Atafaidi nini na ushoga,maandamano, mikutano ya kisiasa isokuwa na tija. Yemba bin Yemba

    ReplyDelete
  2. safi sana , taifa tunaitaji watu wazalendo kama wewe na kuwambia ukweli hawa vibaraka wasio jua mema katika nchi hii, mh jpm achape kazi wafia nchi tupo nyuma yake daima.

    ReplyDelete
  3. Haha unaweza kupata cheo kazana mnec

    ReplyDelete