Mhe Japhet Hasunga (Mb) Waziri wa Kilimo, akikagua ujenzi vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka kabla ya kuzungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, Leo tarehe 5 Januari 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songea).
Mhe Japhet Hasunga (Mb) Waziri wa Kilimo, akikagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka kabla ya kuzungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, Leo tarehe 5 Januari 2019.
Muonekano wa hatua zilizofikiwa za mradi wa ujenzi wa Vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka umaojengwa na Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, Leo tarehe 5 Januari 2019.
Mhe Japhet Hasunga (Mb) Waziri wa Kilimo, akisalimiana na Mwenyeji wake ambaye ni Meneja wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma Ndg Nicodemus Massao wakati alipowasili kwa ajili ya kukagua ujenzi wa vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka kabla ya kuzungumza na wafanyakazi wa NFRA Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, Leo tarehe 5 Januari 2019.
Mhe Japhet Hasunga (Mb) Waziri wa Kilimo, akikagua ujenzi vihenge vya kisasa (Silos) na maghala ya kuhifadhia nafaka kabla ya kuzungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Kanda ya Songea Mkoani Ruvuma, Leo tarehe 5 Januari 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songea
Wakala wa
Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) pamoja na Bodi ya Nafaka na Mazao
Mchanganyiko zimetakiwa kuandaa mikakati ya haraka kuanisha jinsi watakavyo
nunua mazao ya wakulima nchini.
Wakati NFRA
imetakiwa kuainisha namna ya kununua nafaka za wakulima kwa upande wa Bodi ya
Nafaka na Mazao mchanganyiko yenyewe imetakiwa kujikita katika ununuzi wa mazao
mbalimbali ya wakulima ikiwa ni pamoja na kutafuta masoko ya mazao ndani na nje
ya nchi.
Kauli hiyo
imetolewa jana tarehe 5 Januari 2019 na Mhe Japhet Hasunga (Mb) Waziri wa
Kilimo, wakati akizungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya
Taifa ya Chakula (NFRA) mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa
maghala na vihenge vya kisasa.
Alisema
kuwa Wizara yake imekuwa ikihamasisha wakulima nchini kuzalisha kwa wingi mazao
kwa ajili ya chakula na biashara lakini inapofika hatua ya kuuza bei zinakuwa ndogo
jambo ambalo serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe
Magufuli haitalifumbia macho kamwe.
Pamoja na mambo mengine waziri Hasunga
ameupongeza Uongozi wa wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula
NFRA kwa ujenzi wa Maghala na Vihenge vya kisasa (Silos) katika maeneo nane ya
kanda saba za wakala ambapo ujenzi huo utaongeza uwezo wa kuhifadhi mahindi
kutoka Tani 251,000 za sasa hadi Tani 700,000
ifikapo mwaka 2025.
Mradi
huo wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi umeanza kujengwa katika Manispaa ya Songea
(Ruvuma), Dodoma, Mpanda (Katavi), Makambako (Njombe), Mbozi (Songwe),
Sumbawanga (Rukwa), Shinyanga Mjini (Shinyanga), na Babati (Manyara) ambapo
Serikali ya Tanzania na Serikali ya Poland zilisaini mkataba wa mkopo wa
masharti nafuu Septemba 2015 wa Dola milioni 55 sawa na sh. bilioni 124, kwa
ajili ya ujenzi wa mradi huo, ambao utaongeza uwezo wa hifadhi ya chakula.
Mhe
Hasunga amesema kuwa pundi utakapokamilika ujenzi wa maghala na vihenge hivyo utapunguza
gharama mbalimbali zilizokuwa zinatumika kwa ajili ya kununua madawa ya
kufukiza mahindi sambamba na gharama za kununua magunia ya kuhifadhia mahindi.
Katika
hatua nyingine Waziri huyo amemtaka Kaimu Mtendaji Mkuu wa wakala wa Taifa wa
Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba kuweka msisitizo zaidi wa
kununua nafaka ya mahindi kwani katika kipindi chake serikali haitotoa hela kwa
ajili ya ununuzi wa mahindi badala yake NFRA ijipange kibiashara ili iweze
kununua nafaka nyingi na kujiendesha.
Alisema
kuwa huu sio muda wa NFRA kusubiri kupewa mtaji na serikali badala yake
kufikiria tofauti na kuanza kufanya biashara ili kufikia walau ununuzi wa
nafaka kwa Tani zaidi ya 300,000.
Vilevile,
ameutaka Wakala wa majengo Tanzania (TBA) kusimamia kwa weledi mradi wa ujenzi
wa maghala na vihenge vya kisasa ili kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika kwa
wakati ili kuwanufaisha wananchi.
MWISHO.
Ni mwanzo mzuri mh. Wakulima waendelee kupewa elimu kuboresha bidhaa zao kulingana na soko la nje na nchi jirani!
ReplyDelete