Na Stella Kalinga, Simiyu
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally amewashauri Wakuu wa Mikoa hapa nchini
kwenda(kuja) kujifunza namna ya kufanya kazi kwa umoja na mshikamano kati ya
Chama na Serikali sambamba na ubunifu na uchapakazi wa viongozi wa mkoa huo.
Dkt.
Bashiru ameyasema hayo Januari 05, 2019 wakati akizungumza na viongozi na
wanachama wa CCM pamoja na Viongozi na watendaji wa Serikali, Mjini Bariadi
wakati akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu.
Dkt.
Bashiru amewapongeza Viongozi wa Serikali wakingozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka kwa namna wanavyoshirikiana na viongozi wa Chama kwa namna
wanavyosimamia shughuli za maendeleo.
“Niwapongeze
kwa namna mnavyosimamia shughuli za maendeleo, nilikuwa hapa mwaka 2005 kama
msimamizi wa uchaguzi nilizunguka maeneo mengi mengine yalikuwa hayapitiki, leo
nimekuja nikazungushwa maeneo machache tu, nimeona mambo mengi sana ya tofauti
kwa hiyo uongozi wa mkoa huu kwa Chama na Serikali umefanya kazi kubwa na bado
mna nafasi kubwa ya kufanya mambo makubwa zaidi” alisema
Aidha,
amesema ili uchumi uwe imara, wa kisasa na wenye manufaa ni lazima uwe jumuishi
na uwalenge watu walio wengi ambao ni wazalishaji wadogo hususani katika
katika sekta ya kilimo na viwanda huku akisisitiza umakini zaidi ili
uwepo wa viwanda na maendeleo ya kilimo viwanufaishe wengi.
Ameongeza
kuwa wakati Mkoa wa Simiyu unapanga mipango mbalimbali ya maendeleo ya kiuchumi
ni vema kukawa na mpango wa matumizi bora ya ardhi, ili kuondoa migogoro kwa
watumiaji ambayo inakuwa chanzo cha chuki na watu kuishi kwa wasiwasi.
Katika
hatua nyingine Dkt. Bashiru amesema CCM imejipanga kuhakikisha kuwa itasimamia
na kuimarisha ushirika ambao utasimamiwa na wataalam wenye taaluma na maadili
ili uweze kuwanufaisha wanaushirika na kutatua changamoto zao.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema kuwa Viongozi na watendaji wa
Serikali Mkoani humo watahakikisha wanasimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM huku
akisisitiza kuwa fedha zote zinazoletwa katika mkoa wa Simiyu zitasimamiwa
vizuri na zitafanya kazi iliyokusudiwa.
Aidha,
Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu unafanya utafiti kwa kushirikiana na Taasisi ya
Utafiti wa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii(ESRF) ili kubaini fursa za kiuchumi
zilizopo katika katika kila kijiji kwa Vijiji vyote 470, ambapo utekelezaji wa
Falsafa ya Kijiji Kimoja Bidhaa Moja(OVOP) unatarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi
Februari.
Ameongeza
kuwa viwanda vikubwa vitatu vyenye uwezo wa kuajiri takribani wafanyakazi 2000
kikiwepo kiwanda cha chaki na kiwanda cha vifungashio (Maswa) kiwanda cha
bidhaa 18 za afya zitokanazo na pamba(Bariadi) vitajengwa mwaka
huu 2019 Simiyu.
“Ndugu
Katibu Mkuu mwaka jana wakati Mhe. Rais anapokea ndege ya Air Bus alicheza
muziki na ukiangalia ilikuwa ni kitu kinachotoka moyoni kuonesha furaha
yake, ninaamini mwaka 2019 Mhe. Rais ataucheza muziki huo hapa Simiyu” alisema
Mtaka.
Naye
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James ambaye ni Mlezi wa CCM Mkoa wa Simiyu
amesisitiza viongozi na wanachama kuimarisha uhusiano mzuri, kusaidiana na
kupendana katika maisha ya siasa huku akiwasihi viongozi kulinda na kuheshimu
dhamana walizopewa kwa kutimiza wajibu wao.
Akitoa
salamu kwa niaba ya Wabunge wa Mkoa wa Simiyu, Mbunge wa Bariadi,Mhe. Andrew
Chenge ametoa wito kwa viongozi na wanachama wa CCM mkoani Simiyu kudumisha
upendo, umoja na mshikamano hususani katika kipindi cha kueleka uchaguzi wa
Serikali za Mitaa.
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally yuko Mkoani Simiyu kuanzia Januari 05,2019
kwa ziara ya kikazi ya siku mbili yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani
ya CCM mkoani humo.
MWISHO
CAPTIONS:-
PICHA A:-Katibu Mkuu wa CCM Taifa,
Dkt. Bashiru Ally akizungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na
Serikali mkoani Simiyu, katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi Januari
05,2019 wakati wa ziara yake mkoani hapa.
PICHA B:-Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mhe. Kheri James
na Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally wakifurahia jambo katika
kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi na watendaji
wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali mkoani Simiyu, kilichofanyika
Mjini Bariadi Januari 05,2019 wakati wa ziara yake mkoani hapa.
PICHA D:- Katibu Mkuu wa CCM Taifa,
Dkt. Bashiru Ally(wa pili kulia)akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe.
Benson Kilangi mara baada ya kuwasili wilayani humo kuweka jiwe la msingi la
Ofisi ya CCM ya Wilaya, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji
wa Ilani ya CCM mkoani Simiyu Januari 05, 2019 .
PICHA E:- Baadhi ya viongozi wa CCM
wa Mkoa wa Simiyu wakicheza nyimbo za Chama wakati wakijiandaa kumpokea Katibu
Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally(hayupo pichani) katika Mji mdogo wa Lamadi
wilayani Busega, kwa ajili ya kuanza ziara ya siku mbili mkoani hapa Januari 05
na Januari 06 , 2019.
PICHA J:-Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, mhe. Anthony Mtaka akiwasilisha taarifa ya Serikali katika kikao cha
Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi na watendaji wa Chama
Cha Mapinduzi na Serikali mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi
Januari 05,2019 wakati wa ziara yake mkoani hapa.
PICHA L:-Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Mhe. Kheri James
na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo wakifurahia
jambo katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally na viongozi
na watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali mkoani Simiyu
kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05,2019 wakati wa ziara yake mkoani hapa.
PICHA T:-Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,
Mhe. Festo Kiswaga akichangia hoja katika kikao cha Katibu Mkuu wa CCM Taifa,
Dkt. Bashiru Ally na viongozi na watendaji wa Chama Cha Mapinduzi na
Serikali mkoani Simiyu kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05,2019
wakati wa ziara yake mkoani hapa.
PICHA Z4:- Katibu Mkuu wa CCM Taifa,
Dkt. Bashiru Ally(wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
watumishi na viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya k kikao chake
na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali mkoani Simiyu
kilichofanyika Mjini Bariadi Januari 05, 2019.
No comments:
Post a Comment