Tuesday, January 1, 2019

CCM yataka Afrika ikatae kuburuzwa na wakoloni wapya

Azimio la upinzani 

Zanzibar ni mradi wa machafuko Mapya

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro kimesema vyama vya siasa katika mataifa yalioendelea havifanyi mikutano ya hadhara wala maandamano bila vibali mara baada ya chaguzi kuu kumalizika lakini inashashangaza mikutano hiyo ikishinidikizwa ifanyike Barani Afrika.

Kimeeleza maendeleo yaliopatikana  Marekani na ulaya yangekawia mno iwapo wananchi wake wangepuuzia kazi za uzalishaji mali, kujiendeleza kielimu na kundekeza siasa kama inavyotakiwa ifanyike katika nchi za ulimwengu wa tatu .

Msimamo huo umetolewa jana na Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka kwa nyakati tofauti akiwa ameambatana na secretariet ya CCM mkoa wa Morogoro walipofanya ziara ya kukutana na kuzungumza na halamshauri kuu za CCM kata ya Mwembesongo, Mafisa na Kichangani wilaya ya Morogoro mjini mkoani hapa. 

Shaka alisema wananchi wa Afrika wasipobadilika kimtazamo na kifikra ili kutambua umuhimu wa kufanya kazi, kujitegemea na kuacha utamaduni wa kusubiri misaada ya kimaendeleo toka kwa wahisani, Afrika itakumbwa na kadhia ya umasikini usiokwisha na kubaki ombaomba. 

"Uingereza kuna vyama vikuu vya Liberal Domocrat, Consevative na Labour lakini havifanyi maandamano ya ghasia . Hatujakisikia chama cha kijani ( Green Party )na Democratic cha Marekani wakiipinga serikali ya Republican.  Ujerumani kuna CDU, CSU, SPD na FDP navyo havipotezi muda kwa kuitisha maandamano ya ghasia na fujo "Alisema Katibu huyo 

Shaka alimtaka kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo Zitto kabwe kuelewa licha ya maandamano, mikusanyiko na mikutano ya hadhara ni haki lakini inapotolewa amri husika na vyombo vya ulinzi na usalama wa raia, hayupo anayeweza kuhoji na kutengua kwa maslahi mapana ya Taifa . 

Alifahamisha hivi karibuni katika mji Mkuu Paris, Ufaransa wananchi waliandamana kwa nguvu bila kuvijulisha vyombo vya dola na kujikuta wakitiwa mbaroni, kupigwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya uchochezi.

"Nimemsikia kiongozi wa Wanawake ACT Wazalendo akidai watashiriki maandamano na mikutano ya hadhara bila vibali. Namsihi Zitto asiwachuuze watoto wa makabwela, wakiandamana naye asikwepe, tunafahamu  atawakimbia wakati kasheshe zitakapotanda niwaombe sana wakinamama, vijana na makundi yote mkoa wa Morogoro na mikoa mingine puuzeni kauli hatarishi zinazotolewa na vitimbakwiri kama Zito na wenziwe hazitujengi katika amani, umoja na mshikamano " Alisema Shaka.

Akitoa mfano Shaka alisema hata katika Mataifa yalioendelea kiuchumi kwenye mabara ya Marekani na ulaya , shughuli za kisiasa husita baada ya kumalizika chaguzi kuu ili kuwapa nafasi wabunge kujadiliana bungeni na wananchi kufanya kazi. 

"Azimio la Zanzibar ni mradi wa fujo na ghasia kupitia mikutano na maandamano, kuandamana au kukusanyika bila ruhusa ni kosa kisheria, upinzani ujue hata demokrasia nayo ina miiko inayohitaji kuheshimiwa, viongozi wenzangu tunalo jukumu kubwa la kuwaelimisha na kuwakumbusha wananchi wetu wasikubali kuingizwa katika majaribu kwani majuto ni mjukuu"Alieleza.

Katibu huyo wa Mkoa alisema upinzani umebaini utendaji wa serikali ya Rais John Magufuli utapata mafanikio miaka mitano ijayo hivyo watakosa hoja za kuinyooshea kidole serikali na kuilamu hivyo wamepanga njama za kuitisha maandamano hatimae zitokee vurugu na ghasia nchini.

"Viongozi wa upinzani hawana hoja kutokana na utekelezaji mzuri wa ilani ya uchaguzi ya CCM, hawakutegemea utendaji wa serikali zetu zote mbili ungekuwa na kasi kiasi hiki .Walichokitangaza Zanzibar ni azimio la linaloashiria kuleta ghasia na vurugu wanataka yatokee machafuko kama yaliotokea Misri, Syria na Libya" Alieleza Shaka

Aidha alisema wapinzani walifikiri ahadi za Rais Dk Magufuli za kupambana na ufisadi, rushwa na ubadhirifu wa mali za umma , zingemshinda na sasa wanashuhudia miradi ya kimaendeleo ikianzishwa, kukamilika na kuamua kupanga ghasia na machafuko hivyo Tanzania haitakubali iwe nchi ya porojo za kisiasa kila zinapomalizika kampeni na uchaguzi mmoja kwani utamaduni huo ukiruhusiwa, wananchi watapumbaa kifikra na kuwa wavivu wa kufanyakazi, kujituma na kutojitegemea kiuchumi .

"Yalipotokea matatizo kule Pemba watu walioondamana bila vibali vya polisi Januari 26, 27 mwaka 2001, Katibu Mkuu wa CUF Seif Sharif Hamad aliwahamasisha washiriki siku ulipofika akawakimbia majanga yote wakabeba wananchi waliokataa kutii maelekezo ya Serikali, wameanza tena chokochoko eti wanawambia msikilizie kuanzia kesho Januari 1 mimi nawambia kila mkaanga mbuyu atatafuna mwenyewe msiwe na wasiwasi mko katika mikono salama ya ulinzi wa Serikali za CCM tunae Dk Magufuli na Dk Shein hawatakubali hata sekunde kuona amani ya nchi ikichezewa " alisema Shaka. 

No comments:

Post a Comment