Na George Binagi-GB Pazzo
Chama cha
wazalishaji wa mvinyo wa matunda Tanzania (TALMA) kimeiomba Serikali kupunguza
kodi ya ushuru wa bidhaa kutoka shilingi 200 hadi 63 kwa lita moja, hatua
itakayosaidia wazalishaji wa bidhaa hiyo kumudu gharama za uendeshaji.
Ombi hilo
limetolewa na Mwenyekiti wa chama hicho, Adolf Olomi kwenye mkutano wa kifaifa
uliofanyika jana Jijini Mwanza na kuhudhuriwa na taasisi mbalimbali za Serikali
ikiwemo mamlaka ya mapato nchini TRA, shirika la viwango Tanzania TBS pamoja na
Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo SIDO.
Aidha Olomi
alitoa rai kwa wazalishaji wa mvinyo nchini kuhakikisha wanasajili bidhaa zao
ili kufanya kazi kwa mujibu wa sheria ambapo kupitia mkutano huo taasisi na
mamlaka mbalimbali za serikali zilitoa semina namna ya kutekeleza suala hilo.
Nao baadhi
ya wazalishaji wa mvinyo, Straton Mzee kutoka kampuni ya Yande Investment ya
Jijini Mwanza inayozalisha mvinyo wa “Harambee Banana Wine” pamoja na Anna
Barnabas kutoka kampuni ya Bhunu Mbundi ya Jijini Arusha, wamesema kiwango
kikubwa cha kodi ushuru wa bidhaa inahatarisha ukuaji wa wazalishaji wengi wa
mvinyo nchini na hivyo kukwamisha kufikiwa kwa Tanzania ya Viwanda.
Mkuu wa
Idara ya Huduma na Elimu (TRA) Mkoa Mwanza, Lutufyo Mtafya alisema ikiwa
wazalishaji hao wanaona utekelezaji wa kodi ya ushuru wa bidhaa unakuwa mgumu
kutokana na ukubwa wa gharama, wanaweza kuwasilisha serikalini mapendekezo yao
kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho kwa mujibu wa sheria.
Mwenyekiti wa chama cha wazalisha mvinyo kwa kutumia matunda (TALMA), Adolf Olomi akizungumza wenye mkutano wa chama hicho uliofanyika Jijini Mwanza.
Washiriki wa mkutano huo
Tazama Video hapa chini
No comments:
Post a Comment