Sunday, November 25, 2018

SERIKALI YAUKOSOA MPANGO WA UFUNGAJI MGODI WA BUZWAGI

Na George Binagi-GB Pazzo
Serikali imeitaka kampuni ya Acacia kuandaa na kuwasilisha haraka mpango mpya wa urejeshaji mazingira katika hali yake ya kawaida baada ya kusitisha shughuli za uchimbaji dhahabu katika mgodi wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama ifikapo mwaka 2020.


Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko aliyasema hayo jana alipofanya ziara katika mgodi huo kukagua shughuli zinazoendelea mgodi hapo.


Mapema mwaka huu pia Wizara ya Madini ilitaka mpango uliokuwa umeandaliwa na kampuni hiyo kuboreshwa ambapo ulikadiriwa kutumia dola milioni 18 kurejesha mazingira ya mgodi wa Buzwagi katika hali ya kawaida, ikisema mpango huo haukujumuisha kufukiwa baadhi ya mashimo mgodini hapo (tazama picha), bali yabaki wazi hadi yatakapojaa maji katika kipindi cha miaka 100 ijayo. 

Naibu Waziri Doto Biteko (katikati), akifafanua jambo wakati akikagua shughuli mbalimbali katika mgodi wa Buzwagi.
Naibu Waziri Doto Biteko akielekea kukagua sehemu ambapo mchanga wenye madini (makinikia) umehifadhiwa ndani ya mgodi wa Buzwagi.
Tazama Video hapa chini

No comments:

Post a Comment