WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa
*Lengo ni kudhibiti watu wanaoingia nchini bila ya kufuata taratibu
WAZIRI MKUU,
Kassim Majaliwa ameziagiza Kamati za Ulinzi na Usalama kwenye maeneo ya
mipakani kuendesha doria za mara kwa mara ili kuwabaini na kuwachukulia hatua
watu wote wanaoingia nchini kinyemela bila ya kufuata taratibu.
“Suala la
ulinzi na usalama ni muhimu, hivyo Idara ya Uhamiaji kwa kushirikiana na
viongozi wengine wahakikishe wanasimamia sheria na kuimarisha ulinzi hususan
maeneo ya mipakani ili kudhibiti watu mbalimbali wanaoingia nchini kinyemela.”
Waziri Mkuu
alitoa agizo hilo jana jioni (Alhamisi, Novemba 29, 2018) alipozungumza na
wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Stendi ya Ushirombo wilayani Bukombe akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Geita.
Waziri Mkuu
alisema ni muhimu kwa viongozi wa maeneo ya kuwa makini katika kufanya ukaguzi
kwenye maeneo hayo ili wazuie uingiaji wa wageni kiholela kwa sababu baadhi yao
si watu wema. “Serikali haizuii wageni kuingia nchini ila wafuate taratibu
zilizowekwa.
Kadhalika,
Waziri Mkuu aliwaagiza wakuu wa wilaya akiwemo na mkuu wa wilaya ya Bukombe,
Said Nkumba watangaze fursa za uwekezaji zilizopo kwenye maeneo yao kwa lengo
la kuvutia wawekezaji wa sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda ili kukuza uchumi.
Alisema
viongozi hao wawasiliane na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na kuwaeleza
fursa za uwekezaji zinazopatikana katika maeneo yao, ambapo alitolea mfano wilaya
ya Bukombe ambayo ina mifugo mingi, watafute wawekezaji wa kujenga kiwanda cha
nyama.
Pia, Waziri
Mkuu aliwashauri wafugaji nchini kufuga kisasa na kujiongezea tija, badala ya
kutembeza mifugo kwa umbali mrefu wafuge kulingana na ukubwa wa maeneo yao ya
malisho na marufuku kwenda kulisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima.
Mbali na kupiga marufuku wananchi kulisha mifugo
kwenye mashamba ya wakulima, pia Waziri Mkuu amezuia wafugaji kuingiza mifugo
katika mapori ya akiba kwa kuwa mapori hayo kwa sasa yapo katika hatua za
mwisho kutangazwa kuwa mbuga za wanyama.
No comments:
Post a Comment