Na Hamis Abeid
Habari za wakati huu ndugu zangu viongozi, wazazi na waTanzania wote kwa ujumla, ama hakika Mungu ni mwema na anazidi kulibariki Taifa letu hili tukufu lililobarikiwa neema ndogo ndogo na kubwa kubwa ila pia changamoto za hapa na pale. Nawasalimu sana kwa kauli ya amani na upendo.
Kwenye huu waraka wangu mfupi nitazungumza namna gani kama Taifa kwa ujumla tunaweza maliza kabisa hili tatizo la mapenzi ya jinsia moja.
Kwanza kabisa naomba tutambue ushoga kama ugonjwa wa akili *”Mental Illness”* ambao unasababishwa na makuzi ya mtoto pindi akiwa na mwaka 0 hadi miaka 6 maana hapa ndipo huwa kiini kikuu cha tatizo hali mbali na sababu nyingine za kimazingira akiwa mkubwa, hiki kipindi ni muhimu kwa binadamu yoyote na ndipo matatizo mengi yanapoanzia japo watu wengi wanakuwa hawafahamu viashiria vyake ambavyo ukubwani pengine vinaweza kuja kuchagizwa na tamaa zake binafsi ambazo kwa akili ya ugonjwa zinashindwa kujizuia.
Kwa kitaalamu akili ya mwanadamu imepewa vitu vitatu ili kukabiliana na mazingira inaitwa *”THE PSYCHE”* ama *”PSYCHIAC APPARATUS”* ambayo ndivyo vinamfanya binadamu aonyeshe utu wake kutokana na mazingira, vitendo na hali aliyonayo.
Hivyo vitu ni ID, EGO na SUPEREGO ambavyo vyote vinatakiwa kuwa vyenye uhusiano sawa kwenye akili ya mwanadamu ikitokea kimoja kimezidi au kimepungua inakuwa tatizo.
Ngoja nifafanue kidogo, ID hii ni sehemu ya akili ya binadamu ambayo yenyewe huwa haijui kitu kushindwa au kukosa au kutokuweza kama ikitaka kitu au kupenda kitu inalazimisha kukifanya kwa namna yoyote ile hata kama ni baya kwenye jamii husika japo kwenye ID kuna sehemu kuu mbili ambazo ni *EROS* na *THANOTOS* . Hii EROS ndio inatoa nguvu na msukumo wa kufanya mapenzi bila kujali jinsia wala nini, kwa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja hii EROS inakuwa ni kubwa mno akilini mwao. THANOTOS hii huwa inatoa nguvu na misukumo ya mtu kuwa mkorofi, mshari, asie na aibu, pia mtu kupenda vurugu ukizingatia hizo zote ni sifa za watu wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja hivyo kwa hawa watu ID zao huwa ni kubwa kuliko vitu vingine (kutatua hii inawezekana).
EGO hii ni sehemu ya akili ambayo inatambua uhalisia wa mambo mfano mapenzi ya jinsia moja sio halali kwa mazingira yetu, hivyo hii ikiwa ya kutosha akilini itamzuia mtu kujihusisha na hilo tatizo ila ikizidiwa nguvu na ID mtu huwa anajikuta kafanya kitu bila kujijua.
SUPER EGO hii ni sehemu ya akili ambayo inahusika na maadili kwenye jamii husika hii nayo mtu akiishakuwa na ID kubwa huwa inashindwa kufanya kazi na kujikuta mtu anafanya mapenzi ya jinsia moja au kitu chochote cha ajabu licha ya maadili ya sehemu husika kutokuwa upande wake (hili linatatulika).
HATUA ZA MAKUZI YA BINADAMU KUANZIA MWAKA 0 HADI KUFARIKI ZINAZOHUSU MAPENZI/KUPENDA NA NA NAMNA ZINAVYOWEZA PELEKEA UGONJWA WA AKILI NA KIJANA KUANGUKIA KWENYE USHOGA PIA NITAELEZA NAMNA MZAZI ANAVYOWEZA MUEPUSHA MTOTO WAKE
Kabla ya yote tunatakiwa tujue matendo, mienendo na tabia za mtu yoyote ni taswira ya malezi aliyokuwa anapitia kuanzia akiwa na mwaka 0 hadi miaka 6 hivyo kuna vitu vipya vichache sana ukubwani ndani ya pembe kuu tatu za akili ya binadamu.
Hatua za makuzi ni kama ifuatavyo na kila hatua ina namna yake ya kukabiliana nayo ili mtoto wako asipate huu ugonjwa wa akili kwa mujibu wa (Sigmund Freud – baba ya saikolojia ulimwenguni).
1. ORAL
STAGE (mwaka 0 hadi 1)
2. ANAL STAGE (mwaka 1 hadi 3)
3. PHALIC STAGE (miaka 3 hadi 5au6)
4. LATENT STAGE (miaka 5au6 hadi balehe)
5. GENITAL STAGE ( balehe hadi kufa).
1. *ORAL STAGE*
hatua hii ya awali ya makuzi ya mtoto, hapa mtoto anakuwa anatumia mdomo kama kitu pekee kinachomfanya afurahi hivyo kila kitu anakuwa anatumia mdomo kukabiliana nacho hapa atakuwa anakula na kunyonya kila kitu kinachokuwa mbele yake bila kujali nikizuri au kibaya mfano unaweza kuta mwanao anatafuna kandambili (ndala) katika kipindi hiki mtoto anakuwa anamuamini mno mtu anaempa chakula na kumbeba muda wote.
Katika kipindi hiki kama mzazi atashindwa kuwa karibu zaidi na mwanae tunatarajia ukubwani huyu mtoto atakuja kuwa mlevi sugu, mvuta sigara sugu, mlafi wa chakula, mtegemezi, mkorofi na atakuwa na tabia kula kucha hata uzeeni hivyo mzazi unashauriwa kuwa karibu na mwanao.
2. *ANAL STAGE*
Kipindi hiki cha mwaka mmoja hadi miaka mitatu hapa ndipo tatizo linapoanzia.
-kipindi hiki mtoto anakuwa anajisikia raha sana wakati akijisaidia haja kubwa ndomaana muda mwingine unaweza muona mtoto anatabasamu wakati wa haja kubwa hivyo mzazi asipokuwa makini kipindi hiki mtoto atakalili hali hii na kujua kuwa sehemu pekee inayompa furaha ndani ya mwili wake ni sehemu ya haja kubwa na kuendelea kuchezea hizo sehemu hali ambayo itamfanya azoee.
-kipindi hiki mzazi unashauriwa sana kuwa karibu na mwanao muda mwingi kuliko kipindi chote maana ukicheza tu ID yake itamsukuma na kudondokea kwenye hayo mambo pia kwa kipindi hiki usipende kumwacha mtoto wako mashuleni ambako unajua hakuna uangalizi wa moja kwa moja kwa mtoto wako.
× Madhara ya mtoto kukosa malezi bora na ukaribu wa wazazi yanasababisha matatizo makuu yafuatayo:-
a) Ushoga
b) mtu kuwa mvivu mvivu
c) upungufu wa nguvu za kiume
d) kuwa mchafu mchafu
e) kuwa mkorofi na mtukutu.
f) mtu anakuwa na wivu wa kila kitu.
-Mtoto akilelewa vuzuri katika hatua hii anakuja kuwa
mnyenyekevu, msikivu, mpole, msafi pia mtii wa sheria.
-Mzazi kuwa karibu na mwanao kipindi hiki usimuache kwa watu.
3. PHALLIC STAGE
hii ni kuanzia miaka 3 hadi 5 au 6. Hapa mtoto anaanza kujua utofauti wa mvulana na msichana yaani anaanza kutofautisha jinsia na maumbile.
-hapa watoto wa kiume wanaanza kuiga matendo na mienendo ya baba zao huku watoto wa kike wakiiga mienendo ya na matendo ya mama zao.
-lakini pia mtoto wa kiume anakuwa anamuonea wivu baba yake dhidi ya mama yake, uoga wa kupigwa na baba yake kitaalamu tunaita *”Castration anxiety”*.
-lakini pia kipindi hiki mtoto wa kiume anakuwa anapenda kukaa na mama yake kuliko na baba yake wakati mtoto wa kike anakuwa anapenda kukaa na baba kuliko mama yake.
-kipindi hiki baba usipoweka jitihada za kuwa karibu zaidi na mtoto wako wa kiume ni tatizo kubwa sana ataanza kuiga mienendo na vitu kama vya mama yake ambavyo vikishamiri na kuota mizizi kichwani baadae inakuwa tatizo kubwa kulitatua.
-hapa tatizo linakuwa kubwa zaidi kwa watoto wanaolelewa sana na mzazi mmoja hasa mama hivyo mtoto wa kiume muda wote anakuwa na mama hivyo kukosa muda wa kupata simulizi na matendo ya kiume, ikitokea kipindi hiki mtoto yuko na mama muda mwingi anakuwa kwenye hatari kubwa ya kuangukia kwenye janga la ushoga.
×mtoto akikosa malezi bora wakati huu hupelekea matatizo yafuatayo ukubwani kwake:-
a) ushoga
b) ukorofi
c) ubishi
d) kukosa matamanio ya kimapenzi na jinsia ya utofauti na yake.
e) uoga
f) kuwa mtu asie na aibu.
4. *LATENT STAGE*
Hiki ni kipindi cha miaka 5au6 hadi kipindi cha balehe.
-hapa mtoto anaanza kujenga mazoea na watu wengine mtaani au jamii inayowazunguka.
-pia anajifunza vitu mbalimbali kama kucheza mpira, kutengeneza magari, kutengeneza nyumba, michezo ya kibaba mama n.k pia ndicho kipindi anachoanza anza shule.
-kipindi hiki mzazi unatakiwa kuwa makini na mtoto wako kwenye kuchagua aina ya marafiki pia watu wa kuwa nae karibu mtaani na shuleni pia aina ya vipindi vya kuangalia kwenye TV au aina ya magazeti ya kuangalia maana hiki kipindi mtoto anakuwa yuko tayari kujaribu kitu chochote.
5. GENITAL STAGE
Hiki ni kipindi kuanzia balehe hadi mtu anapofariki.
-Hapa mtu anakuwa na hisia kali dhidi ya jinsia tofauti yaani mvulana anakuwa na matamanio ya kimwili dhidi ya msichana na msichana hivyo hivyo.
-ikiwa hatua za awali hazikwenda vizuri hapa utaanza kumuona mtoto wako kama hayuko sawa yaani muda mwingi utamuona ni mpweke lakini pia anakuwa hapendi kuongelea habari za jinsia yake pia muda mwingi anapenda kukaa kukaa na dada zake badala ya kaka zake.
-ukiona hivyo chukua hatua mapema ya kutafuta mtaalamu wa saikolojia akae nae ajue tatizo ni nini kwa haraka (hili tatizo linatatulika).
Hitimisho na mapendekezo yangu
1. Mzazi kuwa makini na makuzi ya mwanao pia kuwa nae karibu muda wote.
2. Kuwa makini na mienendo yake huko mtaani na mashuleni.
3. Kipindi cha utoto usipende kumuacha mtoto wako kwa ndugu au jamaa.
4. Jiupushe kufanya matendo ya ajabu mbele ya mtoto wako.
5. Jiupushe kumpeleka mtoto wako shule za jinsia moja hususani za kulala huko huko.
6. Jenga mazoea ya kuongea na mtoto wako juu ya matatizo yake pia msimulie makuzi yako na michezo ya kipindi chako.
7. Serikali ijenge utamaduni wa kupeleka wataalamu wa saikolojia mashuleni kwa watoto pia sehemu nyingine muhimu kama jela n.k.
8. Wazazi waepuke kuwalaza watoto wao pamoja na wageni ambao sio wakazi wa kudumu wa hapo nyumbani.
Kwa
mawasiliano
Instagram: @hamisabeid
Tel: +255769808725
Email: hamisabeid4@gmail.com
Instagram: @dmsaikolija
Email: saikolojiatanzania@gmail.com
No comments:
Post a Comment