Thursday, November 22, 2018

HII NDIO MIPANGO YA WANA GDSS KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

Wanawake wengi wanaofanya kazi katika sekta zisizo rasmi hasa maeneno ya viwandani wamekuwa wakinyanyasika kwa kutogewa haki wanayostahili, mpaka kufikia kuvaa pampasi wakiwa kazini ili kuweza kukabiliana na changamoto za kimaumbile (wakati wa hedhi) na hata kujisaidia haja ndogo wakati mwingine na hii inatokana kutopewa muda wa mapumziko wakiwa kazini.
 Muwezeshaji wa semina ya Jinsia na Maendeleo Jackson Masawe akitoa ufafanuzi wa jambo fulani mapema wiki hii Makao Makuu ya TGNP Mtandao, Mabibo jijini Dar es salaam. 

Hayo yamesemwa mapema wiki hii na Mwanaharakati Jackson Masawe wakati akiongoza Semina za Jinsia na Maendeleo na mada kuu ikiwa ni  kutokomeza ukatili wa kijinsia katika maeneo ya kazi, na hii ikienda sambamba na kuelekea katika Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia Duniani.

Maadhimisho hayo ambayo ufanyika kila mwaka duniani kote kila ifikapo tarehe 25 mwezi wa 11  na kilele chake kinakuwa ni tarehe 10 ya mwezi wa 12, yenye lengo la kukumbuka matukio kadhaa makubwa yaliyowahi kutokea duniani ambayo yalidhihilisha ukatili wa kijinsia kwa kiwango kikubwa.

Alisema kuwa kauli mbiu ya kitaifa kwa mwaka huu inasema “Usalama wake ni wajibu wangu” hii ikiwa inawalenga waajiri wote kuhakikisha inawajali wafanyakazi wake kwa kuwapa vitendea kazi na kujali usalama wao wakiwa katika maeneo yao ya kazi.

Aliongeza kuwa “Sisi kama wana Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) inabidi tufanye kitu cha tofauti ili kuweza kuleta ukombozi kwa jamii inayonyanyaswa na baadhi ya watu wachache waliopewa mamlaka ya kuongoza wenzao, ikiwa ni miongoni mwa njia za kuenzi siku hizi 16 za kupinga ukatili wa kijinsia duniani”. Alisema Jackson

Na baadhi ya njia zilizopendekezwa na wadau ni kuandaa kongamano kubwa litakalowahusisha wadau mbalimbali kutoka idara za Serikali, Mashirika binafsi pamoja na kuwaalika wasimamizi/viongozi wa viwanda mbalimbali ili kuwapa elimu juu ya haki za wafanyakazi wao na kuwakumbusha wajibu wao kama viongozi.

Lakini pia njia nyingine ni kuandaa Matembezi ya hiari na kusambaza vipeperushi huku wahusika wakiwa na mabango yenye jumbe mbalimbali za kuhamasisha matajiri wanaosimamia shughuli mbalimbali ikiwa ni viwandani, Majumbani, Mashuleni hata Masokoni kujua thamani za wafanyakazi wao.

Na mwisho washiriki wa semina hiyo walihamasishana Kutembelea vituo vya watoto wenye Ulemavu, Yatima ili kujua changamoto wanazokutana nazo pamoja na kwenda hospitalini kujionea ukatili unaofanywa na wauguzi kwa wagonjwa wao.

Mwanaharakati kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Silvia     Sosteness akitoa maoni yake katika mjadala wa Kupinga                  Ukatili wa Kijinsia katika Maeneo ya Kazi.

Baadhi ya washiriki wakifuatilia semina kwa umakini.

Semina ikiendelea.

No comments:

Post a Comment