Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo akihutubia Wahasibu (hawapo pichani) wakati wakiwa katika mafunzo ya Kielektroniki ya Ukusanyaji Mapato ya Serikali mkoani Morogoro.
Mwakilishi wa Chuo cha Mazimbu Campus cha Morogoro, Kundasen Swai akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kulia).
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (katikati) wakijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Idara ya uhasibu, Anthony Tarimo (wa pili kushoto) mara baada ya kufika katika chuo cha Mazimbu Campus kilichopo Mkoani Morogoro.
Na Rhoda James- Morogoro
Naibu
Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amewaeleza wahasibu wa madini nchini kuwa
wizara haitamvumilia mtu yeyote ambaye atakuwa chanzo cha upotevu wa ukusanyaji
wa mapato ya Serekali.
Nyongo
ameyasema hayo wakati akifunga Mafunzo ya Kielektroniki ya Ukusanyaji wa Mapato
ya Serikali ambayo yaliaanza tarehe 12 hadi 15 Novemba, 2018 katika Chuo cha
Mazimbu Campus kilichopo mkoani Morogoro.
Naibu
Waziri Nyongo amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuongeza tija na ufanisi
katika ukusanyaji wa mapato serikalini.
Akizungumza
katika Kikao hicho Nyongo alisema kuwa Viongozi wote wako tayari kutoa msaada
wowote masaa 24 hivyo kama kuna mhasibu ambaye atakuwa na uhitaji kwa masuala
ya kikazi asisite kuwasiliana nao waati wowote.
Aidha,
Nyongo alieleza kuwa tasnia ya uhasibu ni ya muhimu sana katika sekta ya madini,
hivyo ni vyema kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa katika malengo yake
akahakikisha kuwa anafikiria lengo la ndani la Wizara la ukusanyaji wa Bilioni
500 linatimizwa.
Pamoja
na hayo, Nyongo alitoa pongezi kwa wahasibu wote kwa kufanikisha kufikia lengo
la wizara katika ukusanyaji wa mapato ya kiasi cha tsh Bilioni 310 kwa kipindi
cha mwaka 2017/2018 na kuwataka jitihada iliyotumika itumike katika kufanikisha
lengo la muhula huu wa fedha.
Aidha,
Nyongo amemtaka Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Shukurani Manya kuhakikisha
kuwakunakuwa na utekelezaji wa maazimio yote waliyoyafikia katika mkutano huo ili
kuweza kuboresha utendaji wao na kuongeza mapato ya wzara kwa mwaka wa fedha
2018/19.
Akizungumzia
moja ya changamoto walizokuwa wakikutana nazo watumishi wa idara ya uhasibu,
Mkurugenzi wa Idara ya Uhasibu Athony Tarimo alisema ni katika uandaaji wa ripoti
ambayo kwa kupitia mafunzo hayo imepata utatuzi.
Aidha,
amemshukuru Naibu Waziri Stanslaus Nyongo kwa utayari wake wa kukubali kufunga
mafunzo hayo na kwamba anatumaini kwamba
wahasibu hao watakuwa mabalozi wazuri hasa katika kufundisha wengine ambao kwa
namna moja au nyingine hawakuweza kuhudhuria katika mafunzo hayo.
Mafunzo
haya yameshirikisha wahasibu wote wa Wizara ya Madini nchini kote na watumishi
wa takwimu kutoka Madini pamoja na watumishi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment