Tuesday, October 9, 2018

WAZIRI TIZEBA AWATAKA WAKULIMA WA KAHAWA KUENDELEZA IMANI KWA SERIKALI

Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akizungumza kwenye eneo la kiwanda cha Kukoboa Kahawa cha Nkwenda alipopewa nafasi ya kuwasalimia wananchi waliojitokeza kumlaki Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa 
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akizungumza kwenye eneo la kiwanda cha Kukoboa Kahawa cha Nkwenda alipopewa nafasi ya kuwasalimia wananchi waliojitokeza kumlaki Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa

Na Mathias Canal-WK, Kyerwa-Kagera

Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba amewatoa hofu wakulima wa kahawa kote nchini na kuwataka kuwa na imani na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais, Dkt John Pombe Magufuli kwamba haiwezi kumtupa mkulima kwakuwa imejipambanua kuwahudumia watanzania wote juzi tarehe 7 Octoba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal, WK)

Alisema katika kipindi kirefu wananchi hususani wakulima walikosa imani na serikali yao kutokana na uwajibikaji hafifu ikiwemo baadhi ya watendaji kutotekeleza wajibu wao ipasavyo.

Waziri Tizeba alitoa rai hiyo juzi tarehe 7 Octoba 2018 kwenye eneo la kiwanda cha Kukoboa Kahawa cha Nkwenda alipopewa nafasi ya kuwasalimia wananchi waliojitokeza kumlaki Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa wakati akiwa katika ziara ya kikazi Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera.

Alisema kuwa serikali imebaini hujuma walizokuwa wanakumbana nazo wakulima wa kahawa nchini hivyo kubuni mfumo wa uuzaji wa zao hilo kupitia Ushirika eneo pekee litakalowafanya wakulima kujipatia kipato rafiki kutokana na umuhimu wa zao hilo.

Alisema kuwa njia pekee ya kumkomboa mkulima nchini ni pamoja na kuuza kupitia mpango jumuishi wa Ushirika ambao ndio mkombozi wa mkulima.

"Kule Mtwara na Lindi wakulima wa korosho wananufaika na mfumo wa Ushirika kwa kuuza kupitia mnada ambapo wanunuzi wanashindanishwa kwa bei hivyo na huku mwenye Kahawa tutawashindanisha" Alisisitiza Waziri Tizeba na kuongeza kuwa

"Ujanja wa kuwanyonya wakulima sasa ni mwiko, Rais watu amekusudia kuwanufaisha waajiri wake ambao ni wananchi waliompa dhamana nasi wasaidizi wake tutalisimamia hilo kwa kila namna" 

MWISHO.

No comments:

Post a Comment