Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula
(NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba akikagua mahindi wakati wa ununuzi katika kituo
cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula
(NFRA) Bi Vumilia L. zikankuba akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma.
Afisa ubora wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Alfred Jacob Masanja akikagua mahindi kwenye kituo cha ununuzi cha Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma.
Na Mathias Canal, NFRA
Zoezi la kununua nafaka ya
mahindi kwa ajili ya akiba ya Taifa ya Chakula unaendelea katika maeneo
mbalimbali kote nchini ambapo wakulima kwa kiasi kikubwa wameitikia wito
uliotolewa na Wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) wa kutonunua mahindi
yasiyokuwa na ubora.
Pamoja na Ubora wa mahindi kuwa
changamoto katika maeneo mengi nchini kutokana na hali ya msimu wa mwaka Jana
kuwa na jua Kali na mvua za msimu jambo lilolopelekea Mazao kuharibika yakiwa
shambani.
Katika hatua nyingine Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia
L. zikankuba ameendelea na ziara ya kikazi ya kutembelea vituo mbalimbali vya
ununuzi ambapo hivi tarehe 1 Octoba 2018 alitembelea kituo cha ununuzi cha
Kigonsela kilichopo Mkoani Ruvuma kukagua mwenendo wa zoezi la ununuzi katika
kituo hicho.
Katika ziara hiyo ya Mtendaji
Mkuu wa NFRA mkoani Ruvuma, Meneja wa Kanda ya Songea Ndg Amos Mtafya alieleza
kuwa Kanda ya Songea pekee imepangiwa kununua jumla ya tani 7, 000 kwa awamu ya
kwanza ya ununuzi na hadi kufikia leo tarehe 1 Oktoba 2018 Kanda hiyo
imeshanunua zaidi ya tani 6000.
Ili kuimarisha dhana ya
Ushirika, Wakala umenunua kwa kiasi kikubwa mahindi kupitia vyama ya Ushirika
na vikundi vya wakulima yaani SACCOS na AMCOS ambazo jumla yake zinakuwa 23
ambazo ndizo zilizobainishwa na uongozi wa Mkoa wa Ruvuma.
Vikundi hivyo vya wakulima ni
kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, Songea vijijini, Mbinga mji,
Mbinga vijijini, Namtumbo na Wilaya ya Nyasa.
Vumilia aonyesha kuridhishwa na
hali ya ubora wa nafaka iliyonunuliwa na kuwahimiza watumishi wa NFRA kuendekea
kusisitiza na kununua mahindi yenye vigezo vya ubora unaokubalika kwa ajili ya
Hifadhi ya Taifa ya Chakula.
Katika hatua nyingine Bi Vumilia
amewapongeza watumishi wa NFRA kwa kazi nzuri ya kiuweledi wanayoifanya katika
kutekeleza majukumu yao na wakala kwa ujumla.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment