Wednesday, October 10, 2018

MTANDAO WA ELIMU WA TESEApp WAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM


Muanzilishi wa TESEApp Abdul Mombokaleo, akionyesha Tablet ambayo mwanafunzi anaweza kutumia katika kusoma katika mtandao wa TESEA  ikiwa tayari imewekwa mtandao maalumu wa masomo ya sekondari (Kidato 1 - 4) na (kidato 5 - 6) akiwa na  Mwenyekiti wa Taifa wa wamiliki wa shule na vyuo binafsi nchini (TAMONGSCO) Ndugu Charles Totera katika uzinduzi wa TESEApp.

Muanzilishi wa TESEApp Abdul Mombokaleo, akionyesha Tablet ambayo mwanafunzi anaweza kutumia katika kusoma katika mtandao wa TESEA  ikiwa tayari imewekwa mtandao maalumu wa masomo ya sekondari (Kidato 1 - 4) na (kidato 5 - 6) akiwa na  Mwenyekiti wa Taifa wa wamiliki wa shule na vyuo binafsi nchini (TAMONGSCO) Ndugu Charles Totera katika uzinduzi wa TESEApp.
Muanzilishi wa TESEApp Abdul Mombokaleo wa kulia akisalimiana na Mwenyekiti wa Taifa wa wamiliki wa shule na vyuo binafsi nchini (TAMONGSCO) Ndugu Charles Totera katika uzinduzi wa TESEApp.  



Muanzilishi wa TESEApp Abdul Mombokaleo akizungumza katika uzinduzi wa TESEApp.

Baadhi ya wadau elimu na Walimu wa shule mbalimbali jijini Dar es Salaam wakifatilia kwa makini uzinduzi wa mtandao wa elimu wa TESEApp.

Muanzilishi wa mtandao wa Elimu wa Tesea Abdul Mombokaleo amesema kuwa msingi wa kuanzishwa kwa mtandao wa Tesea ni kurahisisha upatikanaji wa marejeo(notes) kwa wanafunzi kujifunza na kupata elimu kwa kutumia teknolojia ya kisasa.


Amesema mtandao huu utakuwa na marejeo(notes) zote za kutosha  na ambayo yame hakikiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania ili kusaidia wanafunzi kupata marejeo yanayotakiwa katika masomo yao.



"mtandao huu hauchukui nafasi ya mwalimu bali utamsaidia mwalimu kuandaa masomo kwa urahisi kwani notes hizo zinafata mtaala wa serikali kwa kuwa na silabasi zote zinazotakiwa kwa mwanafunzi kujifunza awapo shuleni". amesema Mombokaleo



Amesema mtandao huo unaopatika kupitia simu za smartphone,laptop,tablet na computer za mezani na unaweza kupakuliwa kiurahisi na mwanafunzi kijisali na kuanza kutumia mtandao kwa gharama nafuu,na kupata masomo yote ya biashara,sayansi na elimu za dini ya kiislamu na kikristo pamoja na mitihani iliyopita (pastpapers).  



Kwa upande Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Mwenyekiti wa taifa wa wamiliki wa shule binafsi nchini Charles Totera, amesema kuwa elimu inatakiwa kumsaidia mtu kuweza kutatua matatizo yake bila kusubiri msaada kutoka kwa mtu mwingine  kwa uwezo wake wa kufikiri kutokana na elimu aliyonayo.



Amesema kuwa Wizara ya Elimu iache kuwazawadia watu wano karirishwa katika elimu na badala yake kuwapa motisha watu wanakuja na ubunifu ambao unakuwa msaada kwa wengine kwani anafurahi kuona vijana wanatumia tekinolojia kufanya mambo ambayo ni msaada kwa Taifa.



"Elimu ya kukaririsha wanafunzi inaua vipaji na kudumaza akili za wale ambao wanachukia kukariri napiga vita elimu ya kukariri haisadii mtu,nchi wala hata msomi mwenyewe"amesema Totera



Amesema kuwa mtandao huo utasaidia wanafunzi hasa wale ambao wanasoma wenyewe bila mwalimu na ambao hawana vifaa vya kujisomea kupitia mtando huo watapata elimu kamilifu na timilifu na kuwaasa walimu kuacha tabia za kukaririsha wanafunzi kwa ajili ya kufaulu mitihani.


NAMNA YA KUPAKUA NA KUJIUNGA TESEApp
1.Pakua TESEApp kutoka Google play (kupitia Android Devices)
au App Store (kwa iOS Devices)
2. Jiandikishe au jisajili kwa ajili ya kuingia (Sign Up)
3. Chagua Kifurushi Unachohitaji

4. Jifunze na Ufurahie

No comments:

Post a Comment