Friday, October 19, 2018

DKT TIZEBA AMTEUA PROF BENGESI KUWA KAIMU MKURUGENZI BODI YA SUKARI

Prof Kenneth Michael Kitundu Bengesi

Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) amemteua Prof Kenneth Michael Kitundu Bengesi kuwa kaimu Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Sukari Tanzania.

Uteuzi wa Prof Bengesi unaanza leo Ijumaa Octoba 19, 2018.

Awali, Prof Kenneth Michael Kitundu Bengesi alikuwa ni Mhadhiri Mwandamizi katika Idara ya Mipango na Usimamizi wa Sera na Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Jamii na Binadamu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine mkoani Morogoro.

MWISHO.

No comments:

Post a Comment