Tuesday, September 4, 2018

WAZIRI WA KILIMO MHE DKT CHARLES TIZEBA AWASILI NCHINI RWANDA KUSHIRIKI KONGAMANO LA MAPINDIZI YA KIJANI BARANI AFRIKA (AFRICAN GREEN REVOLUTION FORUM –AGRF)

Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba

Na Mathias Canal, Kigali-Rwanda

Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba jana tarehe 4 Septemba 2018 aliwasili Kigali nchini Rwanda kwa mwaliko wa Waziri wa Kilimo na Rasilimali Wanyama wa Rwanda, Rais wa Kikundi cha Washirika wa AGRA na AGRF wa kushiriki Kongamano la Mapindizi ya Kijani Barani Afrika(African Green Revolution Forum –AGRF) litakalofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kigali Convention Centre kuanzia tarehe 05 hadi tarehe 08 Septemba, 2018.

Kongamano hilo lenye kauli mbiu ya “Lead. Measures. Grow: Enabling new pathways to turn smallholders into sustainable agribusinesses” litafunguliwa na kuongozwa na Rais wa Rwanda Mhe Paul Kagame ambapo zaidi ya washiriki 2000 wanatarajiwa kuhudhuria.

Waziri Tizeba amehudhuria mkutano huo ambao ni muendelezo wa yatokanayo na mkutano wa G8 wenye lengo la kufuatilia utekelezaji wa Mipango ya Uwekezaji iliyoandaliwa na cchi mbalimbali kwa ajili ya kuongeza uzalishaji na usalama wa chakula Afrika, chini ya Ubia wa Serikali na Sekta binafsi.

Kongamano la AGRF la mwaka 2018 litatoa fursa kwa Tanzania ya kutathmini na kujifunza utekelezaji na uendelezaji wa sekta ya kilimo kwa vitendo barani Afrika kulingana na ushahidi utakaotolewa na viongozi wenye kuchochea mageuzi ya kilimo na kukifanya kama chombo cha kibiashara chenye faida.

Mkutano huo utajumuisha wawakilishi wa wakulima, viongozi wa sekta ya umma, sekta binafsi, mashirika mbalimbali ya kilimo na biashara kama vikundi vya wakulima na taasisi za kiraia wajasiriamali na wadau wa maendeleo.

MWISHO.

No comments:

Post a Comment