Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Tizeba akizungumza jambo wakati wa kikao cha kazi katika ofisini ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Leo 10 Julai 2018.
Na Mathias Canal-WK, Bukoba-Kagera
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba (Mb) na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage wamewasili Mkoani Kagera kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia 10 Julai 2018 hadi 13 Julai 2018.
Ziara hiyo imeanza kwa mawaziri hao kupokea taarifa Mkoa huo iliyowasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kuhusu sekta ya Kilimo na sekta ya viwanda, biashara Uwekezaji.
Katika ziara hiyo kwa pamoja watakutana na wadau wa kahawa, kutembelea Chama cha msingi Kwarukwazi Wilayani Kyerwa, sambamba na kukutana na wadau wa Kahawa na viwanda vinavyokoboa Kahawa Wilayani Karagwe.
Katika siku ya pili ya ziara hiyo mawaziri hao watatembelea na kuongea na uongozi wa viwanda cha Sukari Kagera, kukutana na wadau wa Kahawa na kutembelea Chama cha msingi cha Kyaka Wilayani Misenyi.
Tarehe 11 Julai 2018 ikiwa ni siku ya tatu ya ziara hiyo mawaziri hao kwa pamoja watakutana na wadau wa Kahawa na kutembelea Chama cha msingi Izigo Wilayani Muleba.
Akisoma taarifa ya Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Mkoa huo Meja Jenerali Mstaafu Mhe Salum Kijuu alisema kuwa Mkoa huo ni miongoni kwa mikoa inayolima zao la Kahawa aina ya Robusta kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na aina ya Arabika.
Alizitaja changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika ngazi mbalimbali za ushirika na pia serikalini kuwa ni pamoja na magendo ya kahawa ya Kagera kwenda nchini jirani, wasiwasi wa wakulima juu ya uwezo wa kifedha wa vyama vya ushirika kumudu kukusanya kahawa yote itakayozalishwa msimu huu.
Aidha, alitaja mkakati wa Mkoa huo kwa kushirikiana na Bodi ya Kahawa Kanda ya Kagera (TCB) kuwa wametoa elimu kwa wadau kwa kukutana na viongozi wote wa vyama vya msingi kwa Wilayani zote, ambapo mafunzo juu ya utaratibu mbalimbali umekuwa ukitolewa kupitia vyombo vya habari kwa kutumia wataalamu husika.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment