Monday, July 23, 2018

CCM YAENDELEA KUWASHA MOTO JIMBONI KWA MBOWE, YAVUNA WANACHAMA WAPYA AKIWEMO DIWANI WA CHADEMA

20 Julai 2018

Bwana Robinson Kimaro Diwani wa Chadema Kata ya Machame Uroki  Wilaya ya Hai amejiuzulu nafasi ya Udiwani, amejivua uanachama wa Chadema na Kujiunga na CCM.

Naye Bwana Baraka Rahimu Nanji Mgombea Udiwani wa ACT wazalendo Kata ya Osunyai Wilaya ya Arusha Mjini amejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha Udiwani Kata ya Osunyai amejivua uanachama wa ACT na kujiunga na CCM pamoja na wanachama wengine zaidi ya 45 kutoka vyama vya Chadema, NCCR na ACT.

Viongozi na wanachama hao wote waliohama vyama vyao na kujiunga na CCM wamepokelewa na Kamaradi Humphrey Polepole Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa  kwenye Mkutano wa hadhara Arusha Mjini  Kata ya Osunyai wakati akimnadi Ndg. Eliherema Amos Nnko Mgombea wa Udiwani wa CCM Kata ya Osunyai

Imetolewa na,

IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

No comments:

Post a Comment