22 Julai 2018
Akiwa katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo Kata ya Makanya, Wilaya ya Same Mkoa wa Kilimanjaro Ndg. Humphrey Polepole Katibu Mwenezi wa CCM amesema CCM itaendelea kuboresha upatikanaji wa huduma za maji safi na salama, elimu na miundombinu ya barabara Wilaya ya Same na kwa kipekee Kata ya Makanya.
Akimnadi Ndg. Ismail Amiri Mbwambo mgombea Udiwani wa CCM Kata ya Makanya Ndg. Polepole amewaomba wananchi wa Kata ya Makanya kukiamini Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kumpatia kura za ushindi mgombea wa CCM kwa kuwa CCM kupitia Serikali yake ina mipango mizuri, Sera nzuri na ipo tayari kuendelea kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama, elimu na miundombinu ya barabara kwa manufaa ya wananchi.
Akifafanua mambo ambayo CCM imeyaahidi kwa wananchi Ndg. Polepole amesema katika suala la kuboresha elimu, miundombinu ya barabara, maji safi na salama, ardhi na machinjio ya mifugo CCM imejipanga kuhakikisha zinapatikana Tshs. Milion 60 kwaajili ya kumalizia ujenzi wa madarasa ya Shule ya upilli, upatikanaji wa Tshs. Milioni 48 kwaajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara ya Chang'oko, Tshs. Milioni 700 kwaajili ya kuhakikisha upatikanaji wa Maji safi na salama, upatikanaji wa Tshs. Milioni 12 kwaajili ya ukarabati wa machinjio ya mifugo na kwamba Chama kitasimamia upatikanaji wa ardhi ya kutosha ili wananchi wapate maeneo ya makazi na shughuli mbalimbali.
*"Hili la maendeleo linawezekana kupitia CCM pekee, tupatieni Ismail Mbwambo, mtu mwenye hekima, busara na muaminifu tuweze kuyakamilisha haya kwa haraka"* amesisitiza Ndg. Polepole
Huu ni muendelezo wa Mikutano ya hadhara ya kampeni za uchaguzi mdogo za Udiwani na Ubunge ambapo CCM imejitanabaisha katika kuuza Sera, mipango na hoja za maendeleo kwa wananchi.
Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
No comments:
Post a Comment