Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma Dkt.James Kiologwe akifafanua jambo kwa Kamati ya Ujenzi wa Kituo cha Mlali leo wakati wa ziara ya ukaguzi wa vituo vya afya kuona maendeleo ya ujenzi, katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma
Timu ya Dodoma wakikagua miundombinu ya Kituo cha afya cha Mlali kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Jijini Dodoma leo wakati wakikagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho leo
.................................................
Wananchi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Jijini Dodoma wamemshukuru Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe
Magufuli kwa ujenzi wa vituo vya afya
208 vilivyojengwa na Seriakli kwa ajili ya kutoa huduma bora za afya nchini.
Wameyasema
hayo mbele ya Kamati ya ufuatiliaji wa ukarabati wa vituo vya afya nchini
kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa iliyofika katika
kituo cha afya cha Mlali kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo
hicho kilichopatiwa shilingi bilioni 400 kwa ajili ya ujenzi huo.
Wananchi
hao wamesema Serikali imetambua shida za wananchi wa hali chini na kuona
umuhimu wa kujenga vituo vya afya nchini
kwa lengo la kupunguza kero za utoaaji wa huduma bora kwa jamii maskini.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Ujenzi wa kituo cha afya Mlali,kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Bw. Abbas
Mkomwa ameishukuru Serikali kwa kutoa
shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kimeweza
kujenga , Nyumba ya Mtumishi, Wodi ya wazazi, Maabara, Jengo la upasuaji na jengo la kuhifadhia
maiti.
Amesema
huduma kama hizi zimekuwa zikifanyika lakini kwa sasa jamii imeweza
kushirikishwa katika kila hatua za awali za ujenzi wa vituo vya afya hivyo
kuweka uwazi kwa jamii na kuona kuwa nao wanawajibu wa kushiriki katika ujenzi
wa miundombinu ya vituo vya afya nchini.
“Kwa
mara ya kwanza Serikali imeweza kushirikisha wananchi katika shughuli za
maendeleo, hii inaonyesha jinsi serikali ya awamu ya tano inavyojdhamini
mchango wa wananchi katika kuleta maendeleo“ AmesemaBw. Mkomwa
Naye
Richard Mgulumu Diwani wa kata ya Mlali ameipongeza Serikali kwa ujenzi wa vituo
vya afya nchini, hasa kituo cha afya cha Mlali ambapo anasema kuwa awali kituo
hicho kilikuwa na wodi chache ambazo zilikuwa hazitoshi kuhudumia wananchi lakini
kwa sasa zimeongezeka jambo ambalo litasaidia kuondoa kero za utoaji wa Huduma
za afya katika Halamashauri hiyo.
Amesema
kuwa Kituo hicho cha afya kimekuwa kikipata wagonjwa wengi kutoka Wilaya ya
Kiteto, Wialaya ya Mpwapwa na Malali hivyo kwa ujenzi huo kutasaidia
kuwahudumia wananchi maskini ambao wamekuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta
huduma bora za afya.
Naye
Mganga Mkuu Hospitali ya Jiji la Dodoma Dkt. James Kiologwe ameipongeza Kamati
ya Ujenzi ya kituo cha afya cha Mlali kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa kituo
hicho na kuonyesha uzalendo wa kusaidia jamii.
Aidha
timu ya Ufuatiliaji wa ujenzi wa vituo vya afya Jijini Dodoma imekagua maendeleo
ya ujenzi wa vituo vya afya vya Mlali, Chamwino, Hombolo na Makole.
No comments:
Post a Comment