Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya na naibu mkurugenzi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya
mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani
(USAID) Malaki Msigwa wakimkabidhi hati ya kimila mmoja ya wananchi wa kijiji cha Mlanda ambaye ni mlemavu
Naibu mkurugenzi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Malaki Msigwa akitoa neo kwa wananchi wa kijiji cha Mlanda wakati wa kutoa hati za kimila
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya na naibu mkurugenzi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Malaki Msigwa wakimkabidhi hati ya kimila mmoja ya wananchi wa kijiji cha Mlanda ambaye alikuwa anawakilisha kundi la wazee
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushirikia zoezi la utoaji wa hati miliki za kimila zilizotolewa na Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID)
Picha ya pamoja baina ya viongozi wa Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID),viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa pamoja na baadhi ya wananchi walikuwa tayari wamepokea hati za kimila
NA FREDY MGUNDA.IRINGA.
JUMLA ya wanakijiji 772 kati ya 1890 wa kijiji cha Mlanda kata ya Magulilwa wilaya ya Iringa mkoani Iringa wamepimiwa maeneo na mashamba yao na kukukabidhiwa hati miliki za kimila zinazotolewa kupitia Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Hati hizo zilikabidhiwa na Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya wakati wa sherehe
fupi za kuwakabidhi hati hizo zilizofanyika kijijini hapo na kuhudhuriwa na
umati mkubwa wa wananchi na wageni mbalimbali walikuwepo katika tukio hilo.
Akizungumza na wanakijiji hao
baada ya kukabidhi hati hizo Masunya alisema kuwa hati hizo zitawasaidia
kutenga maeneo kwa ajili ya matumizi mbalimbali kwa kuzingatia uwezo wa ardhi
kuhimili idadi hiyo na kasi ya ongezeko la watu na mifugo kwa miaka mingi
ijayo.
Masunya aliongezea kuwa,hatua
hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi kwa kuimarisha usalama wa miliki za
ardhi na kuongeza thamani ambayo itawawezesha hata kukopesheka katika taasisi
za kifedha zikiwemo benki.
“Usajili wa ardhi ni muhimu kwasababu unaongeza
ulinzi wa umiliki wa ardhi, unawezesha uwekezaji, unaongeza thamani ya ardhi na
unapunguza migogoro ya ardhi,” alisema Masunya
Masunya aliupongeza mpango huo akisema utasaidia
kupunguza eneo kubwa la ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ambayo
haijapimwa.
Aidha Masunya aliwaomba Feed The Future wautanue
mradi huo angalau ufike umalize kupima vijiji vyote vya Halmashauri ya Wilaya
ya Iringa huku akivikumbusha vijiji
vyote vya wilaya hiyo kuendelea kutoa ushirikiano kwenye miradi ambayo
inasaidia kukuza maendeleo ya nchi.
“Tunataka katika kipindi ambacho Mradi wa
Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa
ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) tuhakikishe tunapima ardhi na
mipango ya matumizi bora na ipimwe ili kila mwenye kipande chake cha ardhi awe
na hati yake,” alisema Masunya.
Alisema kwa kupitia sera hiyo, kutakuwa na
usimamizi zaidi wa ulinzi wa ardhi ya watu masikini ili kupunguza uporaji wa
rasilimali hiyo unaofanywa na matajiri.
“Marekebisho ya sera hiyo ya ardhi yatawezesha pia
kufanyika kwa mrekebisho ya sheria mbalimbali za ardhi ili ziendane na sera na
mazingira ya sasa,” alisema Masunya.
Masunya aliwataka wanakijiji wa kijiji hicho ambao
hawajapimiwa maeneo yao kwa sababu mbalimbali ikiwemo ubishi na migogoro ya
kifamilia kutumia vizuri muda ambao bado mradi huo upo katika wilaya hiyo na
kuhakikisha nao wananufaika na zoezi hilo.
Wanakijiji ambao hawajapimiwa maeneo yao wanaweza
kuendeleoa kuzalisha migogoro ambayo haina tija kwa maendeleo yao na
kusababisha waendelee kuwa masikini kwa kuwa hawatakuwa na dhamana ya kwenda
kukopa.
Awali naibu mkurugenzi wa Mradi wa LTA, Malaki Msigwa alisema
kuwa kijiji cha Mlanda kinajumla ya wananchi 1890 na walio nufaika na Mradi wa
Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa
ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) ni wananchi 772 na
kufanikiwa kutoa jumla ya hati miliki za kimila 1777 ambapo wanaume walikuwa
409 na wanawake 363.
Msigwa aliwapongeza wataalamu wa mradi huo kwa
kuhakikisha wanawasaidia wananchi wa kijiji cha Mlanda kupima maeneo yao na kupata
hati miliki za kimila ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwenye maendeleo ya
kiuchumi.
“Baadhi ya miradi imeibuliwa wakati wa upimaji wa
ardhi hivyo ni fursa sasa kwa wananchi wenyewe kuitumia vizuri ardhi waliyopimiwa
na kupewa hati miliki za kimila na kwa kuwa asilimia fulani kijiji hiki
kimepimwa hivyo wanaweza kuwa kijiji cha mfano kwa kuwapa maendeleo hata
wawekezaji wazuri kwa faida yao” alisema Msigwa
Msigwa alisema kati ya vijiji hivyo 41
vitakavyotayarishiwa mipango ya matumizi bora ya ardhi na kila mwenye ardhi
kupimiwa na kupewa hati miliki za kimila, vijiji 36 vipo wilayani Iringa na
vitano vipo wilayani Mbeya.
“Baada ya kukamilisha zoezi la upimaji mashamba na
urasimishaji wa kijiji chote cha Mlanda, hivi sasa mradi unaendelea na upimaji
mashamba katika vijiji vya mradi ambavyo vipo wilayani Iringa” alisema
Msigwa
Naye diwani wa kata ya Magulilwa Jane Mhangala
aliupongeza Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa
Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) kwa
kuzingatia jinsia wakati walipokuwa wanaendesha zoezi la upimaji ardhi katika
kijiji hicho.
“Hongera sana LTA kwa kuwapa elimu wanawake na
wanaume na kuhakikisha kuwa wanapa haki zao sawa bila kuwa na mgogoro wowote
tofauti na ilivyokuwa hapo awali,maana miaka ya nyuma mwanamke alikuwa
anabaguliwa kwenye kila kitu wala alikuwa haruhusiwi hata kumili ardhi” alisema
Mhangala
Mhangala aliongeza kwa kusema kuwa wanakijiji wa kijiji cha Mlanda baada ya kupata elimu ya kumiliki ardhi
kumepunguza sana migogoro ambayo ilikuwa inaleta chuki kwenye familia.
“Kwa sasa ardhi ya kijiji hiki imepanda dhamani kwa
kiasi kikubwa na tayari ishapimwa na mmepata hati miliki za kimila ambazo
zitawasaidia katika maendeleo yenu ya kiuchumi” alisema Mhangala
No comments:
Post a Comment