Leo Julai 16, 2018 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Mwl Raymond Mwangwala amewasili Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora ambapo amepokelewa na Viongozi wa Chama na Serikali wilayani Nzega na Kuzungumza na wajumbe wa Kamati ya Siasa pamoja na Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya juu ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi CCM 2015 -2020.
Akiwa katika Ofisi za CCM Wilaya ya Nzega Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa amekagua Utekelezaji wa Ujenzi wa Kitega uchumi wa Jengo la Ukumbi Mkubwa wakisasa kwa ajili ya Shughuli mbalimbali zikiwemo Harusi na Mikutano mikubwa na kupongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Viongozi wa Wilaya hiyo.
Leo Katibu Mkuu anatarajiwa kufungua kambi la Mafunzo elekezi kwa Vijana wilayani humo juu ya Masuala ya Itikadi ,Uzalendo pamoja na namna ya Vijana kujikwamua kiuchumi.
Tukutane Kazini
No comments:
Post a Comment