Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Aliyemaliza Muda Wake,Seif Shaban Mohamed (kulia) akimkaribisha ofisini na kumkabidhi vitendea kazi Katibu Mkuu Mpya wa Jumuiya hiyo,Erasto Sima (kushoto) katika hafla fupi ya makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya jumuiya hiyo yaliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Elisa Shunda.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Aliyemaliza Muda Wake,Seif Shaban Mohamed (kulia) akimlaki Katibu Mkuu Mpya wa Jumuiya hiyo,Erasto Sima (kushoto) baada ya kuwasili katika katika ofisi za makao makuu ya jumuiya hiyo yaliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam leo,kwa ajili ya makabidhiano ya ofisi.
VIONGOZI na Wanachama wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameungana kwa pamoja na Katibu Mkuu Mstaafu wa jumuiya hiyo Anayemaliza Muda wake,Seif Shaban Mohamed kumpokea Katibu Mkuu Mpya wa Jumuiya hiyo Erasto Sima katika hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya jumuiya hiyo zilizopo Kariakoo jijini Dar es Salaam leo.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa ofisi Katibu Erasto Sima alisema kuwa mojawapo ya vipaumbele vyake atakavyoenda kuvisimamia katika uongozi wake kwa nafasi hiyo ya utendaji wa jumuiya hiyo ya wazazi taifa atahakikisha anawakumbusha watendaji wenzake wa ngazi ya chini kufuatilia kwa makini ulipaji ada ya wanachama waliomo ndani ya muiya hiyo,pia ataendeleza kwa kufanya usimamizi wa kutosha katika uangalizi wa mali na miradi yote iliyopo ndani ya jumuiya hiyo.
"Tunao wanachama wengi katika jumuiya yetu hivyo nitalisimamia suala hili wanachama wetu walipe mapema ada zao siyo hadi kipindi cha uchaguzi ndo watu waje wawalipie ada kwa kweli hilo silipendi ukiwa wewe ni mwananchama wetu ni heri ujilipie ada mwenyewe lakini pia nitahakikisha nasimamia mali za chama na miradi yotde iliyopo katika jumuiya yetu iendelee zaidi ya hapa ilipo ili kukiongezea chama chetu kipato cha ndani" Alisema Katibu Sima.
Akizungumza kuhusu utofauti wa nafasi aliyokuwepo awali na hivi sasa Katibu Mkuu huyo wa Jumuiya ya wazazi CCM Taifa,Erasto Sima alisema kuwa kwa sasa yeye ni mtendaji hivyo atamshughulikia ipasavyo mtu yoyote atakayetaka kukwamisha utendaji kazi wake na majukumu yake yasiende vizuri.
"Ukiachia nafasi za awali nilizokuwa nimezipitia mimi kwa sasa ni mtendaji jana (juzi) Katibu Mkuu wa CCM Taifa,Dk.Bashiru Ally anakabidhiwa alisema sisi kama watendaji hebu tujikite kwenye utendaji wetu tuache siasa,hivyo sitokubali kuona kwa sababu ya mtu fulani kutokutimiza majukumu yake nitamshughulikia ipasavyo yule ambaye atasababisha majukumu yangu yasiende vizuri kwa hiyo nitajielekeza sana kwenye utendaji"Alisema Sima.
Pia Katibu Mkuu huyo wa Jumuiya ya wazazi Taifa,Erasto Sima amemshukuru Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo anayestaafu,Seif Shaban Mohamed kwa kumkabidhi vitendea kazi na miongozo yote ya ofisi hiyo ameahidi kuendelea kuyafanyia kazi yale aliyoyaacha na kumpongeza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa,Rais Dk.John Magufuli kwa kufanya kazi kubwa sana katika kipindi kifupi katika nchi yetu tangu kuchaguliwa kwake tunatimiza majukumu yake kwa hiyo kuharibu jambo lolote ni kumuangusha rais wetu.
Akikabidhi ofisi Katibu Mkuu Mstaafu wa Jumuiya hiyo ya Wazazi CCM Taifa,Seif Shaban Mohamed alisema kuwa anamkabidhi jumuiya hiyo ikiwa na miradi mbalimbali ambapo mradi mkubwa ni shule 56 za shule ambazo zingine zipo katika hali nzuri na nyingine hazifanyi kazi akasema anaamini kwa kupokezana huko kwa kijiti anaamini katibu huyo mpya atafufua shule ambazo hazifanyi kazi na miradi mingine.
"Naamini njia za kufufua miradi hiyo ipo kikubwa niwaombe watendaji na wafanyakazi wote wamuunge mkono katibu mpya,naishukuru sana jumuiya ya wazazi mimi ni Mpemba natoka Pemba Chakecheke kutoka Zanzibar "anawatania waandishi Chakechake Oyeeee huku akicheka" ikanileta Dar es Salaam ikanipeleka Kigoma,Mwanza lakini nikapelekwa nje Italy,South Afrika nikapelekwa Uchina unanzaje kutoishukuru jumuiya hii lakini zaidi imenikutanisha na watu wa aina mbalimbali nimejifunza mambo mbalimbali kule kwetu Pemba kuna watu wa aina moja ila huku changanyikeni unakutana na waislamu wasio waislamu na makabila mbalimbali ukweli nimejifunza mengi sana" Alisema Mohamed.
Alimaliza kwa kumuahidi mpya kumpa ushirikiano muda wowote atakaomhitaji katika suala lolote liwe ziara au jambo lolote la kiutawala na kuwasisitiza watendaji na wafanyakazi wa jumuiya ya wazazi ccm taifa kumpa ushirikiano wa kutosha katibu huyo mpya katika kutekeleza majukumu ya jumuiya hiyo.
No comments:
Post a Comment