Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo akisalimiana na wanakijiji wa kijiji cha Palangawanu mkoani Njombe.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo akikagua wa Kituo cha Afya Palangawanu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo akikagua ujenzi wa msingi wa jengo la wodi ya wazazi na jengo la upasuaji katika Kituo cha Afya Palangawanu.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo akizungumza na wananchi kwenye ukaguzi wa Kituo cha Afya Wanging'ombe.
Wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo kwenye ukaguzi wa kituo cha Afya Wanging'ombe.
Wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo kwenye ukaguzi wa kituo cha Afya Wanging'ombe.
.........................................................
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo amepongeza ubora wa wajengo yanayojengwa katika kituo cha Afya wanging'ombe Mkoani Njombe.
Jafo ametoa pongezi hizo alipokuwa akikagua ujenzi wa miundombinu inayojengwa katika kituo hicho.
Amewataka wananchi kuendelea kusimamia ubora wa majengo hayo na kuendelea kumuombea Rais John Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwahudumia wananchi wanyonge.
Katika ukaguzi huo, Waziri Jafo amemuagiza mhandisi wa halmashauri ya wanging'ombe kusimamia viwango ili majengo yote yakamilike yakiwa katika ubora wa hali ya juu.
Naye, Mbunge wa Jimbo la wanging'ombe Mhe. Greyson Lwenge ameishukuru Sana serikali kwa ujenzi wa kituo hicho cha afya sambamba na kutenga fedha kiasi cha shilingi billion 1.5 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya.
Aidha waziri Jafo alitembelea kijiji cha Palangawanu kuona ujenzi wa kituo cha afya unaoratibiwa na wananchi wenyewe ambapo aliridhishwa sana na kazi kubwa iliyofanywa kwa nguvu za wananchi.
Kutokana na kazi nzuri inayofanywa na wananchi wa Palangawanu Waziri amewataka wananchi wengine hapa nchini kuiga mfano huo.
No comments:
Post a Comment