Tuesday, June 5, 2018

JAFO APIGA MARUFUKU MAMLUKI KUSHIRIKI UMISSETA NA UMITASHUMTA

Na Mathew Kwembe 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amewataka Wakuu wa Mikoa kuhakikisha kuwa mikoa yao inapeleka wachezaji wanafunzi watakaoshiriki mashindano ya UMISSETA iliyoanza leo katika viwanja vya chuo cha Ualimu Butimba kilichopo jijini Mwanza.


Aidha amewataka waamuzi watakaochezesha mashindano hayo pamoja na yale ya UMITASHUMTA kuhakikisha kuwa wanachezesha michezo hiyo kwa kuzingatia kanuni na sheria bila kuwepo upendeleo ili washindi wa michezo yote wapatikane kwa haki.


Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Waziri Jafo alieleza kuwa mashindano ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) yaliyoanza leo yatafanyika yataendelea hadi hadi Juni 15 mwaka huu.


Mashindano ya UMISSETA yatafuatiwa na michezo ya UMITASHUMTA ambayo yatafanyika katika viwanja hivyo hivyo kuanzia tarehe 17 juni 2018 hadi tarehe 29 juni 2018.


Waziri Jafo alieleza kuwa michezo hiyo inatarajiwa kufunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa katika uwanja wa CCM Kirumba hivi karibuni.


 Kwa mujibu wa Mhe.jafo, jumla ya wanamichezo 3,360 watashiriki mashindano hayo wakitokea mikoa 28 upande wa Umisseta, 26 Tanzania Bara na miwili ya Zanzibari, huku Umitashuta mikoa 26 ya Tanzania Bara tu.


Kwa upande wa Umisseta michezo itakayochezwa ni pamoja na soka kwa wavulana na wasichana, netiboli kwa wasichana, wavu kwa wasichana na wavulana, mpira wa mikoni, mpira wa kikapu, riadha maalumu(watu wenye ulimavu).


Mingine ni Riadha ya kawaida, mchezo wa bao kwa wavulana, sanaa za maonyesho (kwaya, ngoma, mashairi, ngonjera) na mpira wa meza.

No comments:

Post a Comment