Friday, June 15, 2018

GAIRO WAMKWAZA JAFO

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo akipokea taarifa ya ukarabati wa kituo cha afya Gairo.
  Ukaguzi wa majengo yanayo jengwa kituo cha Afya Gairo ukifanywa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo 

............................................................................................

Halmashauri ya wilaya ya Gairo Leo imemkwanza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo kutokana na kuonyesha ugoi goi katika utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa Kituo cha Afya Gairo kilichopokea sh.Milioni 400. 

Kituo hicho ni miongoni mwa vituo vya afya 208 vinavyoboreshwa na serikali kwasasa.  

Akiwa mkoani Morogoro leo, Jafo amefika kituoni hapo na kukuta kazi ikiendelea lakini kasi ya ujenzi haikumridhisha waziri huyo.

Waziri Jafo amesema "Halmashauri ya Gairo ukilinganisha na wengine waliopewa fedha hizo mwezi Decemba lakini wenzenu wengi wapo katika umaliziaji lakini nyie hata bati hawajaanza kuweka,".

 Kutokana na hali hiyo, Jafo ameelekeza kuongezwa kwa mafundi na Juni 23,  2018 atafika tena kukagua kama wamebadilika katika kutimiza majukumu yao ya usimamizi wa ujenzi. 

Aidha waziri Jafo amezikumbusha halmashauri zote nchini kukamilisha ujenzi wa vituo hivyo kabla  Juni 30, 2018.

No comments:

Post a Comment