Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakulima wa pamba katika kijiji cha Msai wilaya ya Iramba akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Singida kutembelea vituo na kujionea ununuzi wa pamba, Picha Zote Na Mathias Canal, WK
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza na wakulima wa pamba katika kijiji cha Msai wilaya ya Iramba akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Singida kutembelea vituo na kujionea ununuzi wa pamba, Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe Emmanuel Luhahula.
Kituo cha ukusanyaji na ununuzi wa pamba katika kijiji na Kata ya Msai, Wilayani Iramba
Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe Emmanuel Luhahula akitoa salamu za shukrani kwa Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba kwa kufanya ziara ya kuwatembelea wakulima wa pamba katika kijiji cha Msai wilaya ya Iramba akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Singida kutembelea vituo na kujionea ununuzi wa pamba,
Na Mathias Canal-WK, Singida
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba amemuagiza Mrakibu wa
polisi Wilaya ya Iramba ASP Magoma Mtani kumkamata aliyekuwa mwenyekiti wa Bodi
ya Chama cha ushirika (AMKOS) Msai.
Waziri Tizeba ametoa agizo hilo jana 9 June 2018 Mara baada ya
kutembelea kitongoji cha Kati, Msai na Mtoa akiwa katika ziara ya kikazi ya
Siku mbili kwa ajili ya kutembelea vituo vya ununuzi wa pamba na kujionea msimu
wa ununuzi wa zao hilo katika vijiji hivyo.
Dkt Tizeba amelaani vikali ufujaji huo wa fedha za wakulima huku
akimtaja Paul Ramadhan Kurwa kuhusika na ufujaji huo wa shilingi milioni 23
huku akiendelea kuonekana mtaani pasina kuchukuliwa hatua za kisheria.
"Wakati muelekeo wa serikali yetu inayoongozwa na Rais wetu
Dkt John Pombe Magufuli ukijipambanua kutaka kuboresha maisha ya watanzania
kupitia Kilimo lakini kuna watu wanataka kurudisha nyuma juhudi hizo, hakika
tutawapa kibano kweli kweli hakuna utani kwenye fedha za wananchi"
Alikaririwa Dkt Tizeba
Mhe Tizeba ametoa siku moja kukamatwa kwa mwizi huyo na kufikishwa
mahakamani ili awe mfano kwa wezi wengine wasio kuwa na haya wala soni.
Aidha, amewataka wananchi katika msimu huu wa uuzaji na ununuzi
wa Pamba kutouza Pamba zenye uchafu wakidhani wataongeza idadi ya kilo kwani
kufanya hivyo ni kufifihisha juhudi zao wenyewe jambo ambalo halina tija.
Sambamba na hayo pia amewaondoa hofu wakulima kote nchini kuwa
serikali ya awamu ya tano inatekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi ya Chama
Cha Mapinduzi yenye mkataba na wananchi katika kipindi cha miaka mitano
2015-2020.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe Emmanuel Luhahula
amempongeza Waziri Tizeba kwa kutembelea maeneo mbalimbali ili kujionea ununuzi
wa Pamba huku akiwasihi wananchi wilayani humo kulima kiasi kikubwa cha Pamba
msimu ujao kwani mbegu na madawa ya kuulia wadudu vitatolewa bure kuanzia msimu
ujao wa mwaka 2018/2019.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment